Msanii
wa Kizazi Kipya (Bongo Fleva) Ndugu Haji Noorah ambaye Kimziki/Sanaa
anafahamika kwa Jina la Noraah A.K.A Baba Stylez(Starz) akizungumza na
Vyombo vya Habari kuhusiana na Mwenendo wa Afya Yake.
===*****===
Habari
Kwanza Blog imekutana na Msanii Noorah kujua hali ya Afya yake"Kimsingi
naendeea Vizuri kwa sasa,Nilikuwa nimelazwa Hospitali ya
Kairuki(Mikocheni Mission Hospital) kwa tatizo la Tumbo,Nimekuwa
nikizumbuliwa na Tumbo kwa Muda wa miaka 20 nikidhani ninatatizo la
Vidonda vya tumbo kumbe ndivyo Sivyo,Baada ya Vipimo vya Madaktari
wamegundua ninatatizo kwenye Utumbo wangu,hivyo wameshaanza kunifanyia
Matibabu na hali yangu imeendelea Kuimarika kadri ya siku zinavyo
kwenda".Alisema Noorah.
Hit Maker
wa Lugha Gongana Noraah anaongeza "Rai yangu kwa Watanzania na Wasanii
wote tuwe na tabia ya Kufanya Uchunguzi wa Afya Zetu,Mimi nimekuwa na
tatizo hili kwa Muda wa miaka 20 nikidhani ni tatizo la kawaida tu,baada
ya kupima nimegundulika na tatizo kwenye Utumbo wangu,nashukuru Mungu
sana Madaktari wamefanya kazi kupitia Operesheni ya Tumbo,hivi sasa
naendelea Vizuri".
Noorah
amewashukuru sana Wasanii wote na Watanzania wanaoendelea kumuombea na
kumjulia hali yake,Hii inaonesha ni nanma gani Wasanii tunatakiwa kitu
kimoja wakati wa Shida na Raha.
Rais
wa Shirikisho la Mziki Tanzania Ndugu Addo Novemba Mwasongwe
akizungumza na Vyombo vya habari mara baada ya Kuwasili na Ujumbe wake
Nyumbani kwa Msanii Noorah kwaajili ya Kumjulia hali yake na kutoa
mchango wao kwaajili ya Afya ya Msanii Noorah.Rais wa Shirikisho la
Mziki
Tanzania
amesisitiza Umoja miongoni mwa Wasanii wakati wote,Shirikisho linaomba
Wasanii kusaidiana katika Shida na Raha,"Tumekuaja kumuona Noorah
kwasababu ni Mwanamziki Mwenzetu na amekuwa bega kwa bega kwenye sanaa
yetu,Shirikisho linatoa Rai kwa Wasanii na Watanzania kuja kumuona
Msanii mwenzao hapa Nyumbani,kumjulia hali na hatimaye Uwe utamaduni
wetu kwa Wasanii wote tunapopatwa na Matatizo."Alisema Addo.Makamu
wa Rais wa Shirikisho la Mziki Tanzania Ndugu Samwel Braiton alimaarufu
Braiton Mtz na Mmiliki wa Backyard Reckords akizungumza na Vyombo vya
Habari nyumbani kwa Msanii Noorah hii leo alipofika kwaajili ya Kumjulia
hali.Kubwa zaidi Braiton amewaomba Wasanii kujenga Utamaduni wa
Kusaidiana na Kujuliana hali,haitakuwa afya sana hadi mtu apate tatizo
kubwa sana ndipo watu waanze kujitokeza"Nawasanii Wasanii wote tuungane
katika hali yoyote na tujenge utamaduni wa kujuliana hali". Rais
wa Shirikisho la Mziki Tanzinia Ndugu Addo Novemba Mwasongwe akikabidhi
Mchango wa Fedha Taslimu Laki tano kwa Msanii Noorah hii leo walipofika
Nyumbani kwake kwaajili ya Kumjulia hali yake ya Kiafya.Ujumbe
kutoka COSOTA,Kushoto ni Philemon Kila Ofisa Msajili wa Umiliki kazi za
Wasanii,katikati Msanii Noorah na Kulia ni Ofisa kutoka COSOTA
anayeshughulikia Teknolojia na Mawasiliano.
Hapa
ni Mkurugenzi wa Habari Kwanza Media/Blog Ndugu Sanga Festo akiwa
katika Picha ya pamoja na Msanii Noorah baada ya Kumtembelea Nyumbani
kwake Sinza-Darajani hii leo.
Hivi Sasa
Noorah anaendelea na Matibabu katika Hospital ya Mikocheni(kairuki) kwa
mfumo wa Kliniki na anatarajia kuhudhuria Kliniki baada ya wiki mbili
kaunzia sasa.Jumla ya Gharama zake za Matibabu hadi sasa zimefikia
Milioni 2.7,Wasanii/Watanzania mnaomba kuungana na kutoa sapoti yenu kwa
ndugu Yenu na Msanii wenu Noorah katika kipindi hiki cha Kurejesha afya
yake katika hali ya kawaida iliaendelee na majukumu ya Kila siki katika
sanaa na Maisha yake binafsi.
Picha na Habari kutoka kwa Sanga Festo wa Habari kwanza Media/blog