Baadhi
ya wakurugenzi wa bodi ya Manchester United wameshindwa kuvumilia
matokeo mabaya ya klabu na kuamua kumgeuka kocha David Moyes wakitoa
ishara kwa mara ya kwanza kwamba ni muda sasa umefika wa kumtimua kocha
huyo, taarifa kwa mujibu wa jarida la Fanzine Red, ambalo lina ukaribu
na klabu hiyo.
Familia
ya Glazer sasa wapo radhi sasa kupokea wazo la kubadilisha kocha, ingawa
mpaka sasa bado wanampa sapoti Moyes, lakini wiki ijayo inasemekana
mambo yanaweza kubadilika. United kesho inabidi ifanye kila liwezekanalo
kubadilisha matokeo ya 2-0 dhidi ya Olympiakos katika Champions League,
baada ya hapo wataenda kupambana na timu ngumu ya West Ham United
halafu siku chache baadae wanakutana na mahasimu wao Manchester City.
Wakati
endapo wataweza kufuzu kucheza robo fainali ya Champions League
kutaleta ahueni kwa Moyes, matokeo mabaya ya kutolewa na kuelekea mechi
zingine ambazo kama hatopata matokeo mazuri basi mambo yanaweza
kumbadilikia. Uvumilivu utawashinda mabosi wa familia ya Glazers.
Inaaminika
The Glazers wapo katika presha kubwa hasa baada ya mfululizo wa matokeo
mabaya hivi karibuni, huku maofisa wengine wa bodi ya wakurugenzi
tayari wameshaanzisha hoja ya kufanyika mabadiliko kwenye benchi la
ufundi.
Vyanzo
vya habari Old Trafford vinaripoti kwamba imeonekana hata Sir Alex
Ferguson haonekani kumsapoti Moyes hadharani katika mikutano ya bodi,
ingawa pia bado hajambadilika mrithi wake. Hata hivyo Moyes bado
anasapotiwa na Bobby Charlton.
Wakati
huo huo mtandao wa gazeti la The Sun umeripoti kwamba David Moyes
amepewa mechi 3 - dhidi ya Olympiakos, Westham United na Manchester City
na endapo atapoteza mechi 2 kati ya hizo basi ataondolewa na Ryan Giggs
atakaimu nafasi yake mpaka msimu ujao utakapoanza mchakato mpya wa
kutafuta kocha wa kudumu.