Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akipokea salama ya heshima kutoka Jeshi la Polisi
kabla ya hotuba ya uzinduzi wa Bunge maalum la Katiba leo mjini Dodoma.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akikagua gwaride liliandaliwa na Jeshi la Polisi
kabla ya hotuba ya uzinduzi wa Bunge maalum la Katiba leo mjini Dodoma.
Mwenyekiti
wa Bunge Maalum la Katiba Samwel Sitta (kulia) na Makamu Mwenyekiti
Samia Suluhu wakijadiliana jamba nje ya ukumbi wa Bunge kabla hotuba ya
uzinduzi wa Bunge Maalum la Katiba leo mjini Dodoma.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutuba Bunge Maalum la Katiba wakati wa sherehe za uzinduzi wa Bunge hilo leo mjini Dodoma.
Makamu
wa kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Maalim Mh. Seif
Sharif Hamad (kushoto) Jaji Mkuu wa Zanzibar Mh. Omar Othman
Makungu(Katikati) na Rais Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
Dkt. Amaan Abeid Karume Wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa Hotuba ya Uzinduzi wa
Bunge Maalum la Katiba Mjini Dodoma Leo.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa
katika picha ya Pamoja na Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba Leo Mjini
Dodoma.
(Picha na Idara ya Habari-MAELEZO)
===***===
DAKIKA 155:46 ZA HOTUBA YA RAIS JAKAYA KIKWETE KWA WAJUMBE WA BUNGE MAALUM LA KATIBA, AMEMALIZA KAZI KWENU WAJUMBE
===***===
DAKIKA 155:46 ZA HOTUBA YA RAIS JAKAYA KIKWETE KWA WAJUMBE WA BUNGE MAALUM LA KATIBA, AMEMALIZA KAZI KWENU WAJUMBE
Rais
Jakaya Kikwete, akiwahutubia Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba leo
katika ukumbi wa Bunge mjini Dodom, ambapo katika hotuba yake ametumia
dakika 155:46, kwa kutoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali yahusuyo muundo
wa Katiba mpya ikiwa ni pamoja na kufafanua kuhusu shinikizo la muundo
wa Serikali tatu na mambo kadhaa ya Muungano
.
.
Wajumbe wakinyanyuka kwa pamoja na kupiga makofi kumshangilia Rais Jakaya, baada ya kukonga kwa Speech yake.
Sehemu ya Wajumbe waliohudhuria .....
Sehemu ya Mabalozi waliohudhuria ufunguzi huo wa Bunge la Katiba katika ukumbi wa Bunge mjini Dodoma leo jioni.
Mama
Maria Nyerere (katikati) Mama Siti Mwinyi (kushoto) na Mama Salma
Kikwete, wakiwa ukumbi humo wakimsikiliza Rais Jakaya Kikwete.
Mke
wa Makamu wa Rais Mama Asha Bilal (kushoto) Mama Tunu Pinda na Mama Asha
Seif Balozi, pia wakifuatilia hotuba hiyo kwa makini.
Rais Jakaya Kikwete, akikagua gwaride maalum kabla ya ufunguzi rasmi wa Bunge hilo.
Badhi ya waandishi wa habari wapiga picha wakiwa bize.
Mwenyekiti
wa Bunge Maalum la Katiba, Samuel Sitta na Makamu wake, Samiah Suluhu,
wakijadiliana jambo wakati wakisubiri kuwapokea viongozi.
Waandishi na watu mbalimbali wakiwa nje ya ukumbi huo wakati wa maopokezi ya viongozi mbalimbali.
Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Ummy Mwalimu, akiwasili kwenye viwanja vya bunge.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwasili kwenye viwanja vya Bunge.
Mwenyekiti wa Bunge la Katiba, Samuel Sitta, akiwasili kwenye viwanja vya Bunge.
Baadhi ya waandishi.....
Mhe James Mbatia akiwasili na mjumbe mwenzake Mhe Kamili
Picha zote na Ofisi ya Makamu wa Rais.