Kamanda
wa Polisi, Kanda Maalumu Dar es Salam, Suleiman Kova alitaja majina ya
Wanaijeria hao kuwa ni Sunday Chaidikaobi (42), Chukwuma Favour (31), na
Franklin Indubuisi (41). Mtanzania aliyebambwa pamoja na Wanaijeria hao
ametajwa kuwa ni bi Hadija Ngoma (43), mkazi wa Kimara Temboni, Dar es
Salaam.
RAIA
watatu wa Nigeria na mwanamke wa Kitanzania wamekamatwa na polisi jijini
Dar es Salaam, wakituhumiwa kujaribu kusafirisha madawa ya kulevya
kwenda nchini Liberia. Watuhumiwa hao wanadaiwa kuwa walikuwa mbioni
kutuma mihadarahi hiyo, ikiwa kwenye vitabu, kwa kutumia Wakala wa
Usafirishaji Mizigo ya DHL.
Kwa
mujibu wa Kamanda Kova, polisi walipata taarifa juzi, Machi 18, kuwa
kuna watu wanne wanajihusisha na usafirishaji wa dawa za kulevya
waliokuwa katika ofisi za DHL zilizopo Barabara ya Sam Nujoma.
Kufuatia
taarifa hizo, Kamanda Kova amesema “makachero walifuatilia suala hilo na
hatimaye siku hiyo saa 8:30 mchana watu hao walikamatwa wakiwa na
kifurushi wakijiandaa kukisafirisha kwenda nchini Liberia.”
Alisema
polisi walipopekua kifurushi hicho, walikuta vitabu vitatu vya
Kiingereza. Walipopekua vitabu hivyo, walikuta madawa aina ya heroin
katika kurasa za mwanzo.
“Katika
vile vitabu kurasa ya kwanza inayofunika lile jalada gumu kwa ndani,
walikuwa wamefunua na kuweka unga huo na katika ukurasa wa nyuma vivyo
hivyo kwa vitabu vyote,”aliongeza.
Unga huo
unaokadiriwa kuwa na uzito wa nusu kilo, umepelekwa kwa mkemia mkuu wa
serikali kwa uchunguzi zaidi kubaini thamani na uthibitisho wa madawa
hayo.
Miezi
kadhaa iliyopita, Wanigeria wawili walikamatwa katika uwanja wa ndege wa
kimataifa wa Jomo Kenyatta nchini Kenya, wakijaribu kusafirisha dawa za
kulevya aina ya cocaine zenye thamani ya takriban shilingi milioni 120;