Meneja Uhusiano wa Kituo cha
Uwekezaji Tanzania (TIC) Pendo Gondwe, akizungumza na kituo cha Tv1
baada ya mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo kwenye ukumbi wa
MAELEZO jijini Dar es Salaam.
Meneja Uhamasishaji wa Uhamaishaji
wa kituo hicho John Mnali akizungumza na waandishi wa habari kuhusu
mafanikio ya kituo hicho katika kuhamasisha uwekezaji wa ndani leo
kwenye ukumbi wa MAELEZO jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Meneja Uhusiano
wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC)Pendo Gondwe.
Meneja Uhusiano wa Kituo cha
Uwekezaji Tanzania (TIC)Pendo Gondwe (katikati) akizungumza na waandishi
wa habari kuhusu mafanikio ya kituo hicho katika kuhamasisha uwekezaji
wa ndani leo kwenye ukumbi wa MAELEZO jijini Dar es Salaam.Kushoto ni
Meneja Uhamasishaji wa Uhamaishaji wa kituo hicho John Mnali na kulia ni
Afisa Habari wa Idara ya Habari-MAELEZO, Frank Mvungi.
Mwandishi
wa Habari kutoka gazeti la The Citizen, Henry Mwangonde akiuliza jambo
wakati wa mkutano kati ya Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) na
waandishi wa habari uliofanyika kwenye ukumbi wa Idara ya Habari
(MAELEZO) leo jijini Dar es Salaam.Picha na Hussein Makame-MAELEZO.
--
Na Frank Mvungi- Maelezo
KITUO cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimefanikiwa kusajili miradi 9,442 tangu kuanzishwa kwake hadi 2013.
Hayo yamesemwa na Meneja Uhusiano wa TIC, Pendo Gondwe wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.
Gondwe
alisema kuwa Watanzania wamekuwa na muamko katika uwekezaji ambapo
katika miradi yote miradi ya Watanzania ni asilimia 52 na 25 ni miradi
inayomilikiwa kwa ubia kati ya wageni na watanzania.
Aliongeza
kuwa asilimia 23 ni miradi iliyowekezwa na wageni kutoka mataifa
mbalimbali ambapo alisema miradi ambayo inaongoza kwa uwekezaji ni
Kilimo, Maliasili, Miundombinu, Nishati, viwanda na biashara,
Usafirishaji, Elimu, Afya, Miundo mbinu na madini.
Alisema TIC inawahamasisha Watanzania kujitokeza kuwekeza katika miradi mbalimbali ili kusaidia katika kukuza uchumi wa Taifa.
Gondwe
alisema TIC imekuwa na utaratibu wa kuhamasisha wananchi kushiriki
katika uwekezaji katika sekta nmbalimbali ambapo kituo hicho kimekuwa
kikitumia mikutano na makongamano kuhamasisha wananchi kusajili miradi
yao.
Kituo
cha uwekezaji kinatoa huduma mbalimbali kwa ajili ya wawekezaji wa
ndani kupitia dirisha moja yaani ONE STOP CENTRE ikiwemo kuandikisha
kampuni, kujisajili na VAT, TIN, na leseni mbalimbali.