Wafanyabiashara
ya Madini ya mchanga,kokoto na mawe Jiji la Mbeya wameandamana kwenda ofisi ya
Mkurugenzi wa Jiji kwa kutumia maroli kupinga waraka wa Wizara ya Nishati na
Madini unaowataka watumiaji wa bidhaa hiyo kulipia shilingi elfu mbili mia tano
kuanzia Machi 3 mwaka huu.
Maandamano
hayo yalipokelewa na Mkurugenzi wa Jiji Mussa Zungiza ofisini kwake ambapo
alikana kutoa waraka huo na kufafanua kuwa waraka huo umetolewa na Wakala wa
Ukaguzi wa Madini[Tanzania Minerals Audit Agency-TMAA].
Akitoa
malalamiko yao mbele ya Mkurugenzi Bwana nidhamu wa wachimbaji na wasafirishaji
bidhaa hizo Peter Hezron N’gwavi amesema kuwa kitendo cha tozo na leseni
kitafanya vijana waliojiajiri kuanza kufanya vitendo vya uhalifu kutokana na
ukosefu wa mitaji.
Mkurugenzi
wa Jiji amesema kuwa madai yao hayahusu ofisi yake bali wenye dhamana ya kujibu
kero hizo ni mamlaka husika ambayo ni Wizara ya Nishati na Madini hivyo
atawaomba wawakilishi wao waweze kujibia kero zao.
Mhandisi wa
Jumanne Mohammed ambaye ni Afisa Mfawidhi ofisi ndogo ya TMAA Mbeya amesema
kuwa waraka wa kulipia bidhaa za Mchanga,Kokoto na Mawe ulipitishwa na Bunge
Mwaka 2010 ndipo ulipoanza kutumika rasmi kwa tozo la asilimia 3 kwa bei ya
bidhaa iliyopo Sokoni.
Hata hivyo
Mohammed amesema kuwa leseni za uchimbaji wa bidhaa za ujenzi hazihusiani na
madereva wanaobeba bidhaa hiyo
hivyo wao wanapobeba bidhaa hizo wanapaswa kupata kibali kuoka kwa mmiliki wa
mgodi wa madini hayo ambapo kibali hicho hutolewa bure katika ofisi yake
iliyopo eneo la Mwanjelwa Jengo la IFAD.
Alimaliza
kwa kuwataka wanaotaka kufanya biashara hiyo wafuate taratibu za kisheria ili
kuepusha migogoro isiyo ya lazima kwani hali hiyo inaikosesha Serikali pato
halali linalotokana na watu wachache wanaojinufaisha bili kufuata taratibu.
Na Mbeya yetu
|
0 comments:
Post a Comment