SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Sunday, February 16, 2014

UNYAMA HUU ANAOFANYIWA MTOTO HUYU


OFM yamuokoa mtoto wa huyu.
Huu ni zaidi ya unyama! Mama ambaye ni mwalimu wa shule ya msingi huko Tandika, Dar, almaarufu kwa jina la Mama Kumburu, anatuhumiwa kwa unyanyasaji wa kijinsia wa mtoto wa miaka 10 kisha kutiwa mbaroni.

 Baada ya kupata malalamiko ya raia kuwa kuna mtoto anatumikishwa kazi za mtu mzima, hivi karibuni Timu ya Oparesheni Fichua Maovu (OFM) iliingia mzigoni na kwenda kumwokoa mtoto huyo ambaye ni mwanafunzi wa darasa la pili wa shule ya msingi huko Temeke.
 Awali, OFM ilifika nyumbani kwa mama huyo maeneo hayo ya Tandika ili kujiridhisha na tuhuma hizo ambapo ilijionea jinsi mama huyo anavyomtumikisha na kumnyanyasa mtoto huyo.
 Kwa mujibu wa majirani, mtoto huyo ambaye yupo chini ya umri wa miaka 18, huamshwa saa 11:00 alfajiri na kutakiwa kufanya kazi zote za ndani (isipokuwa kupika) na kwenda kuchota maji kwa mkokoteni kila siku, tena umbali mrefu huku ikidaiwa kuwa hufanya hivyo mara tatu au nne kwa siku bila kula.

Mtoto huyo akichoteshwa maji.

 Kama hiyo haitoshi, ilidaiwa kuwa mara kwa mara mtoto huyo hupewa kipigo kikali kwa makosa ya kawaida, kiasi cha majirani kukerwa na vitendo hivyo na kumuomba mama huyo aache mara moja tabia hiyo lakini hakusikia.
 Ilidaiwa kwamba siku moja kabla ya kukamatwa kwa mwalimu huyo, mtoto huyo alipokea vipigo mfululizo kisa alimsindikiza jirani yake aliyeomba aende naye mahali.
Siku ya tukio OFM ilimtafuta mtoto huyo ambapo ilimkuta akijiandaa kwenda shule na kujionea jinsi alivyodhoofu na kujaa makovu mwilini.

Mama mtuhumiwa almaarufu kwa jina la Mama Kumburu (wa pili kutoka kushoto) akipelekwa polisi.

 OFM ilimfuatilia mtoto huyo hadi shule anayosoma na kujionea jinsi maendeleo yake kimasomo yasivyoridhisha huku akijitenga na wenzake na kuwa mtu mwenye wasiwasi na huzuni muda wote.
Majira ya saa 11:00 jioni, OFM, ikiwa na polisi wa dawati la jinsia kutoka Mbagala-Kizuiani ‘iliseti’ mitego yake kila kona na kupata taarifa kuwa shangazi wa mtoto huyo ambaye ndiye anayedaiwa kuhusika na unyanyasaji huo, alikuwa tayari amerejea kutoka kazini hivyo kwa muda huo mtoto huyo angeanza kufanyishwa kazi ikiwemo kuchota maji jambo ambalo lilikuwa kweli.
 Haraka, OFM ilimfuatilia mtoto huyo akiwa na tolori la maji lenye madumu manne hadi bombani ambapo mwenyewe alisema aliambiwa na shangazi yake, arudie kuchota maji mara nne, jambo ambalo lilikuwa kweli.
 OFM ilimshuhudia mtoto huyo akijaza madumu ya maji na kulisukuma tolori hilo kwa tabu huku kila aliyemuona akiishia kumsikitikia jambo lililowalazimu OFM wamsaidie huku wakiongozana na polisi hao hadi nyumbani kwao na kumkamata mama huyo.
 Akionesha ubabe wake, mwanamama huyo awatolea maneno machafu OFM  na polisi waliokuwa eneo hilo na kudai kuwa yeye anafahamiana na watu wakubwa na kamwe hawezi kwenda rumande.



Hata hivyo, baada ya kuona mambo yanakuwa magumu, mama huyo alikubali kuelekea kituoni ambapo alifunguliwa jalada la kesi namba MBL/RB/1827/2014- UNYANYASAJI huku mtoto huyo akiwekwa chini ya uangalizi wa ustawi wa jamii.
NA GPL

0 comments:

Post a Comment