SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Wednesday, January 29, 2014

Picha:Aliyewahi Kuwa Mbunge wa Jimbo la Ulanga Magharibi na Waziri wa Viwanda na Biashara, Mh. Juma Ngasongwa anusurika ajalini huko kibaha,mkoani pwani

  Mh Juma Ngasongwa akikokotwa kuingizwa Hospitali ya Tumbi kupatiwa matibabu baada ya kupata ajali katika eneo la Kibaha jana jioni. Mhe. Ngasoma amenusurika kifo katika ajali hiyo iliyotokea jana jioni Kibaha Picha ya ndege Mkoani Pwani
 Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mwantumu Mahiza na Dr Loti Kiwelu akimjulia hali katika Hospitali ya Tumbi Kibaha alipofikishwa kwa ajili ya huduma ya kwanza ambapo alihamishiwa katika Hosipitali ya Muhimbili MOI kwa ajili ya matibabu zaidi.
  Ajali hiyo ilihusisha gari  aina ya Rav 4 mali ya Ngasongwa ambaye alikuwa akiendesha mwenyewe kutoka jijini Dar es salaam kuelekea Morogoro ambapo kwa mujibu wa Ngasongwa alichomekewa na lori la Tanesco pichani chini.
 Gari la Ngasongwa likiwa limeharibika vibaya.
 Lori la Tanesco lililosababisha ajali hiyo.Picha na Chris Mfinanga

0 comments:

Post a Comment