Mkurugenzi
wa Uchumi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Morrice Oyuke ametoa wito
huo wakati akizungumza na vyombo vya habari leo jijini Dar es salaam
kutoa taarifa ya fahirisi za uzalishaji wa bidhaa za viwandani hadi
kufikia mwaka 2012 zilizowekwa katika makundi mbalimbali kwa kufuata
mwongozo wa Umoja wa Mataifa.
Mtafiti
na mtaalam wa Uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam Prof. Haji
Semboje akizungumza wakati wa mkutano huo leo jijini Dar es salaam.
Pamoja na mambo mengine amesema juhudi zinahitajika katika kuwahamasisha
Watanzania kumiliki viwanda vidogo, vya kati na vile vikubwa.
Sehemu ya waandishi wa habari kutoka vyombo vya habari wakati wa mkutano huo leo jijini Dar es salaam.
Na. Aron Msigwa, Dar es salaam.
Wito
umetolewa kwa watanzania kujitokeza kwa wingi katika kuanzisha na
kumiliki viwanda vitakavyozalisha bidhaa mbalimbali hapa nchini kwa
lengo la kuongeza ajira, kukuza pato la taifa na kupunguza hali iliyopo
ya uagizaji wa bidhaa mbalimbali toka nje ya nchi.
Mkurugenzi
wa Uchumi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Morrice Oyuke ametoa wito
huo wakati akizungumza na vyombo vya habari leo jijini Dar es salaam
kutoa taarifa ya fahirisi za uzalishaji wa bidhaa za viwandani hadi
kufikia mwaka 2012 zilizowekwa katika makundi mbalimbali kwa kufuata
mwongozo wa Umoja wa Mataifa.
Amesema
kuwa ongezeko la viwanda nchini licha ya kuongeza ajira kitakwimu lina
mchango mkubwa katika kusaidia kupima fahirisi za uzalishaji wa bidhaa
za viwandani na kuongeza kuwa uzalishaji wa bidhaa za viwandani hupima
mabadiliko ya kiasi cha bidhaa zilizozalishwa na wazalishaji mbalimbali
ambao kwa wastani wamejiajiri kuanzia wafanyakazi 50 na kuendelea.
Amefafanua
kuwa Tanzania katika kipindi cha mwaka 2006 hadi 2012 imekua na kiwango
cha juu cha mabadiliko ya fahirisi ya bei ya uzalishaji wa bidhaa za
viwandani kwa jumla ya asilimia 10.8 ikilinganishwa na asilimia 2.1 za
mwaka 2011.
Ameongeza
kuwa fahirisi za uzalishaji wa bidhaa za viwandani kwa mwaka 2012
zimeongezeka na kufikia 328 ikilinganishwa na 296 za mwaka 2011 na
kuongeza kuwa ongezeko hilo limechangiwa na uzalishaji wa vinywaji na
tumbaku kwa asilimia 16.8%, Viwanda vya chuma 14.6% na ongezeko na
bidhaa za nguo na ngozi kwa asilimia -17.7%.
Bw.
Oyuke ameyataja makundi mengine yatokanayo na bidhaa za viwandani kuwa
ni pamoja na Mbao na bidhaa za mbao 0.3%, Karatasi na bidhaa za karatasi
5.0%, Kemikali, Petroli na bidhaa za Plastiki -7.9%, Bidhaa za udongo,
vioo na bidhaa zisizo za metaliki 7.5% na bidhaa zitokanazo na chuma
11.0% .
Naye
mtafiti na mtaalam wa Uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam Prof.
Haji Semboje akizungumza wakati wa mkutano huo amesema kuwa mfumo wa
uzalishaji na biashara nchini unatokana na uwepo wa bidhaa za Kilimo na
zile zisizo kuwa za kilimo na kuongeza kuwa juhudi kubwa zinahitajika
katika kuwahamasisha Watanzania kumiliki viwanda vidogo, vya kati na
vile vikubwa.
“Bado
tunakabiliwa na changamoto ya umiliki wa viwanda hapa nchini kwa sababu
viwanda vingi vikubwa vinamilikiwa na wageni, watanzania walio wengi
wanamiliki viwanda vidogo vidogo” amesema Prof. Semboje.
Ameongeza
kuwa hivi sasa kuna ongezeko kubwa la bidhaa mbalimbali zikiwemo nguo
kutoka nje ya nchi jambo ambalo linaathiri uchumi wa ndani na kusisitiza
kuwa kuwa juhudi zinahitajika katika udhibiti wa bidhaa zisizokidhi
viwango na ambazo hazina chapa ya eneo zilikotengenezwa ambazo
zinapatikana katika masoko ya Tanzania.
Prof.
Semboje ameeleza kuwa kutokana na kuongezeka kwa uwezo wa watanzania
kununua, kuagiza na kufanya biashara nje ya nchi ipo haja ya watanzania
hao na serikali kwa ujumla kupitia mamlaka husika za uwezeshaji
wananchi kiuchumi kuangalia uwezekano wa kuwajenga uwezo wa kununua
mitambo inayozalisha bidhaa hizo na kuileta ndani ya nchini kwa lengo
la kuongeza pato la taifa na kuwawezesha wananchi kiuchumi.
“
Ninapenda kutoa wito kwa Taasisi za Uwekezaji nchini kutoa kipaumbele
kwa Watanzania katika suala la uwekezaji wa ndani pia kutoa elimu zaidi
kwa watanzania katika uzalishaji wa kisasa kwa sababu tayari serikali
imeshaweka mipango mizuri ya kuwaendeleza watanzania, changamoto
tuliyonayo ni kuitafsiri mipango na sera zilizopo kwa manufaa ya nchi”
0 comments:
Post a Comment