Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Pereira Silima(katikati)
akitoa taarifa ya Mafanikio ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi katika
kipindi cha Serikali ya Awamu ya Nne kwa Waandishi wa Habari(hawapo
pichani) leo Januari 21, 2014 katika Ukumbi wa Mikutano, Makao Makuu ya
Jeshi la Polisi, Jijini Dar es as Salaam(kulia) ni Kamishna wa Utawala
wa Jeshi la Polisi, Clodwing Mtweve(Kushoto) ni Mkurugenzi Mkuu wa Idara
ya Habari na Maelezo, Bw. Assah Mwambeni.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini, John Casmir Minja akiwa
pamoja na Viongozi Wengine Wakuu wa Idara zilizo chini ya Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi wakati Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mhe. Pereira Silima akitoa taarifa rasmi ya Mafanikio ya Wizara ya Mambo
ya Ndani katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Nne(wa pili kulia) ni
Kamishna Mkuu wa Idara ya Uhamiaji, Sylivester Ambokile(kushoto) ni
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Nchini, Pius
Nyambacha.
Baadhi ya Wakurugenzi mbalimbali wa Idara za Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi wakifuatilia kwa makini taarifa ya Mafanikio ya Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Nne iliyotolewa
na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Prereira Silima kwa
Waandishi wa Habari leo Januari 21, 2014 katika Ukumbi wa Mikutano,
Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, Jijini Dar es Salaam.Picha zote na Lucas
Mboje wa Jeshi la Magereza
0 comments:
Post a Comment