Naibu Katibu Mkuu ,Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Ahmad Kassim Haji
Mjumbe Mpya wa Kamisheni ya Utumishi wa Umma Bi. Rukia Mohamed Issa
----
STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY ZANZIBAR
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein
jana amewaapisha Nd. Ahmed Kassim Haji kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya
Makamu wa Pili wa Rais na Bibi Rukia Mohamed Issa kuwa Mjumbe wa
Kamisheni ya Utumishi wa Umma nchini.
Kuapishwa
kwa watendaji hao kunafuatia uteuzi wao uliofanyika hivi karibuni
ambapo Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
alimteua pia Dk. Mohamed Seif Khatib kuwa Mwenyekiti wa Baraza la
Kiswahili Zanzibar.
Miongoni
mwa viongozi waliohudhuria hafla hiyo ya kuapishwa ni pamoja na Makamu
wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi, Jaji Mkuu wa Zanzibar Mheshimiwa
Omar Makungu, Spika wa Baraza la Wawakilishi Mheshimiwa Pandu Ameir
Kificho, Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Omar Saleh Kabi, Katibu Mkuu
Kiongozi Dk. Abdulhamid Yahya Mzee, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mji wa
Zanzibar Mheshimiwa Khatib Abdulrahman Khatib na Mkuu wa Mkoa wa Mjini
Magharibi Abdalla Mwinyi Khamis.
Postal Address: 2422 Tel.+255 776 613 015, Fax: 024 2231822
0 comments:
Post a Comment