Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji.
Na Nicodemus Jonas
MWENYEKITI wa Yanga, Yusuf Manji, jana alimjia juu Katibu wa Baraza la Wazee wa klabu hiyo, mzee Ibrahim Akilimali, akimtaka kuacha kujifanya msemaji wa Yanga.
MWENYEKITI wa Yanga, Yusuf Manji, jana alimjia juu Katibu wa Baraza la Wazee wa klabu hiyo, mzee Ibrahim Akilimali, akimtaka kuacha kujifanya msemaji wa Yanga.
Manji alimbwatukia mzee huyo hadharani katika Mkutano Mkuu wa Yanga
uliohudhuriwa na zaidi ya wanachama 400 kwenye Ukumbi wa Karume, PTA
Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti huyo ambaye alionekana kuchachamaa, alimlaumu mzee huyo
kwa kumshambulia kipa Juma Kaseja, kisa kikiwa ni kufungwa kwenye mchezo
wa Nani Mtani Jembe dhidi ya Simba ambapo
Yanga ililala kwa mabao 3-1 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
“Tafadhali naomba tuheshimiane, wewe ni mzee wangu, nilikukuta Yanga ukanibeba, hivyo tii katiba, waachie wasemaji wafanye kazi yao,” alisema Manji huku akiwataka wale wote wasiohusika na mamlaka ya Yanga kukaa kimya na kuacha kuyaongelea masuala ya klabu kwenye vyombo vya habari.
Huku wengi wakiwa hawajategemea, Manji alisema hayo mbele ya wanachama waliohudhuria mkutano huo na kusisitiza ukweli na uwazi ndiyo jambo bora.

“Nimesema hapa, watu wote wamesikia na wewe kama mzee wetu naamini
umeelewa na utajirekebisha,” alisema Manji ambaye baadaye alikutana na
Mzee Akilimali, akampa mkono na kumkumbatia, hali iliyoonyesha
wameelewana.
Akizungumzia sakata hilo, Mzee Akilimali alisema: “Nimeupokea vizuri
ushauri wa Manji na ametupa uhuru zaidi kwa kuwa kama tutakuwa na maoni
yetu, tutakuwa tunapeleka kwa uongozi husika juu ya kipi kifanyike.”
Mkutano ulipangwa kuanza saa 3:00 asubuhi na ulikuwa na ulinzi wa
hali ya juu kutoka kwa vyombo vya usalama. Zaidi ya askari 15 wa Jeshi
la Wananchi Tanzania (JWTZ) na mbwa wanne walikuwa wametapakaa kila kona
ya ukumbi huo.
Ukumbi huo ulikaguliwa na mbwa wa polisi kabla ya mkutano kuanza, vilevile kulikuwa na vifaa maalum vya kubaini silaha.
Mgeni rasmi, Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal
Malinzi, aliingia saa 5:00 asubuhi, akiambatana na Mjumbe wa Baraza la
Wadhamini la Yanga, Mama Karume na baadaye akawapongeza Yanga kwa
kuendesha mkutano kwa utulivu.
Kwa upande wake Mjumbe wa Bodi ya Udhamini, Francis Kifukwe, alizungumzia suala la uwanja ambapo alisema:
Kwa upande wake Mjumbe wa Bodi ya Udhamini, Francis Kifukwe, alizungumzia suala la uwanja ambapo alisema:
“Tumeingia mkataba na kampuni ya Kichina ya BCEG tangu Novemba 2012.
Tayari Wachina wametekeleza majukumu yao kwa kuleta michoro ya usanifu
wa awali ya kiwanja hicho, lakini wameshindwa kuanza kutokana na eneo
dogo kwani wanataka eneo la hekta zaidi ya 15.
“Ni uwanja wenye uwezo wa kubeba watu 40,000 na wa kisasa. Tumeiomba serikali na Manispaa ya Ilala ili ituongeze eneo, baada ya kulipa deni tulilokuwa tunadaiwa tangu 1972, zaidi ya shilingi milioni 100.

“Tunataka uwanja huo uwe na eneo la maegesho, hoteli, kumbi za
mikutano, sehemu za starehe na benki za wanachama. Baada ya kila kitu
kukamilika, tumepanga kubadilisha jina la Jangwani.
“Kuna mtu aliiba hati miliki ya klabu. Anaitwa (anamtaja), aliiba hati Juni 24, 2009. Inadaiwa alikuwa mjumbe ndani ya Yanga, ndiye aliyesababisha deni hilo la zaidi ya Sh milioni 100.
“Kuna mtu aliiba hati miliki ya klabu. Anaitwa (anamtaja), aliiba hati Juni 24, 2009. Inadaiwa alikuwa mjumbe ndani ya Yanga, ndiye aliyesababisha deni hilo la zaidi ya Sh milioni 100.
“Baraza la udhamini limemfuatilia mpaka ailipe hiyo fedha lakini
anakuwa mgumu, hivyo tunafuatilia kuhakikisha anachukuliwa hatua za
kinidhamu.”
Pia baadhi ya wanachama wa Yanga, walitoa kali pale walipopiga magoti
na kumuomba Manji kuendelea kuwa mwenyekiti, lakini akashikilia msimamo
wake wa kutogombea kama alivyotangaza awali huku akisisitiza muhimu ni
kujadili maendeleo ya Yanga katika mkutano huo.
Aidha, katika mkutano huo, wanachama wa Yanga waliiomba kamati ya
utendaji kuwaruhusu kumchangia Mrisho Ngassa lile deni lake la TFF
ambapo Sanga amewaomba wawasilishe michango yao kwa katibu mkuu.
0 comments:
Post a Comment