Katibu Mkuu wa CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akihutubia mkutano wa hadhara katika kijiji cha Msanga, Wilaya ya Kisarawe.
Katibu Mkuu wa CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akihutubia mkutano wa hadhara katika kijiji cha Msanga, Wilaya ya Kisarawe.
Naibu
Mkurugenzi wa Haki za Binadamu, Habari na Uenezi wa CUF Taifa bw. Abdul
Kambaya, akihutubia mkutano wa hadhara katika kijiji cha Msanga, Wilaya
ya Kisarawe.
Katibu Mkuu wa CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akikabidhi baiskeli kwa nd. Khamis Salum mwenye ulemavu, mkaazi wa Kisarawe.
Wasanii wakitoa burdani kwenye mkutano wa CUF uliofanyika kijiji cha Msanga Wilayani Kisarawe.
Baadhi ya wananchi wakifuatilia mkutano wa CUF uliofanyika kijiji cha Msanga Wilayani Kisarawe. (picha na Salmin Said, OMKR).
Katibu
Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad,
amewashauri wananchi wa Kisarawe kuachana na vyama vilivyopoteza
muelekeo, na badala yake kukiunga mkono chama chenye dira ya kuwaletea
maendeleo.
Amesema
hatma ya maendeleo ya wananchi iko kwa wananchi wenyewe, na kwamba ndio
wenye maamuzi ya kuchagua uongozi wanaoutaka kwa maendeleo yao na taifa
kwa jumla.
Akizungumza
na wananchi hao kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya
Msanga sokoni Wilaya ya Kisarawe, Maalim Seif amesema mabadiliko ya
kiuongozi yanahitajika katika kuwakomboa wananchi kiuchumi na kijamii.
Amesema
ni jambo la kushangaza kuona Tanzania imeachwa nyuma kimaendeleo katika
kipindi cha miaka 53 ya uhuru, huku nchi nyengine zilizokuwa hadhi sawa
na Tanzania zikipiga hatua kubwa za maendeleo.
Amezitolea
mfano baadhi ya nchi zilizopiga hatua kubwa kimaendeleo kuwa ni pamoja
Singapore na Malaysia, nchi ambazo zilikuwa maskini kuliko Tanzania, na
kwamba Tanzania ina mengi ya kujifunzo kutoka nchi hizo.
“Singapore
na Malaysia zilikuwa nchi maskini kuliko nchi yetu, lakini sasa zamepaa
hadi dunia ya pili kuelekea ya kwanza kwa maendeleo. Hii imetokana na
uongozi na mipango bora ya maendeleo waliyojiwekea”, alifafanua Maalim
Seif.
Amefahamisha
kuwa kitu cha kushangaza ni kuona Tanzania ina rasilimali nyingi zaidi
kuliko nchi hizo lakini imedumaa kimaendeleo, jambo ambalo linapaswa
Watanzania walitafakari kwa kina na kulitafutia ufumbuzi muafaka.
Amesema
iwapo chama cha CUF kitapewa mamlaka ya kuongoza dola, kitahakikisha
kuwa kinaunda serikali ya Umoja wa Kitaifa Tanzania, ili kutoa fursa kwa
wataalamu wa Itikadi tofauti za vyama vya siasa kushiriki katika
serikali na kuwa kichocheo cha maendeleo.
“Nani
mwana uchumi mzuri Tanzania kuliko Profesa Lipumba, lakini maskini
hayumo kwenye serikali kwa sababu tu ni mpinzani, sasa sisi tukipata
serikali hatutofanya makosa kama hayo”, alihoji na kusisitiza.
Mhe.
Maalim Seif ambaye ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar ametumia hiyo
kuwaeleza wananchi wa Kisarawe juu ya mafanikio yaliyopatikana Zanzibar
tangu kuanzishwa kwa mfumo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa.
Amesema
kuundwa kwa serikali hiyo kumetokana na maamuzi ya wananchi wengi wa
Zanzibar, na kuwabeza wale wanaoubeza mfumo huo ambao pamoja na mambo
mengine umerejesha amani, umoja na mshikamano miongoni mwa Wazanzibari.
Ametaja
mafanikio mengine ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa kuwa ni pamoja na
kuongezwa kwa bei ya karafuu kutoka shilingi elfu tatu hadi elfu 15 kwa
kilo moja, pamoja na kupunguzwa kwa gharama za pembejeo za kilimo.
Mapema
akizungumza katika mkutano huo, Naibu Mkurugenzi wa Haki za Binadamu,
Habari na Uenezi wa CUF bw. Abdul Kambaya amesema bado Wilaya ya
Kisarawe inakabiliwa na matatizo ya miundombinu ya barabara, elimu na
afya.
Amewashajiisha
wananchi wa Wilaya hiyo kubadilisha mfumo wa uongozi, ili kuwezesha
rasilimali za nchi ziweze kutumika vizuri kwa maslahi ya wananchi wote.
Kabla
ya mkutano huo Mhe. Maalim Seif alifanya ziara ya kichama katika Wilaya
hiyo na kufungua matawi ya CUF, pamoja na kukabidhi baiskeli ya matairi
matatu kwa ndugu Khamis Salum mwenye ulemavu, ili iweze kumsaidia katika
harakati zake za kimaisha.
Hassan Hamad, OMKR.
0 comments:
Post a Comment