Mwakilishi
wa Kampuni ya ukaguzi ya ACM Tanzania Tawanda Manyuchi (kushoto)
akipeana mkono na Meneja Mwandamizi wa Benki ya Exim – Mafunzo na
Maendeleo Priti Punatar kabla ya kukabidhi cheti cha kimataifa cha ubora
wa viwango cha ISO kwa kituo cha mafunzo cha benki hiyo jijini Dar es
Salaam mwishoni mwa wiki. Akishuhudia wapili kushoto ni Meneja Msaidizi
Mafunzo na Maendeleo Japhet Kemboi. (Picha na mpiga picha wetu).
Afisa
Fedha Mkuu wa Benki ya Exim Selemani Amani (katikati) akizungumza na
waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki wakati wa
hafla ya kupokea cheti cha kimataifa cha ubora wa viwango cha ISO
kilichotunukiwa kwa kituo cha mafunzo cha benki hiyo. Kutoka kushoto ni
Meneja Msaidizi Mafunzo na Maendeleo Japhet Kemboi na Mkuu wa kitengo
cha kudhibiti Majanga wa Benki ya Exim David Lusala.
Afisa
Fedha Mkuu wa Benki ya Exim Selemani Amani (katikati) akionyesha moja
ya machapisho ya mawasiliano ya benki hiyo kwa waandishi wa habari
jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki wakati wa hafla ya kupokea cheti
cha kimataifa cha ubora wa viwango cha ISO kilichotunukiwa kwa kituo cha
mafunzo cha benki hiyo. Wakishuhudia ni Meneja Msaidizi Mafunzo na
Maendeleo Japhet Kemboi (kushoto) na Mkuu wa kitengo cha kudhibiti
Majanga wa Benki ya Exim David Lusala (kulia).
Mwakilishi
wa Kampuni ya ukaguzi ya ACM Tanzania Tawanda Manyuchi (kushoto)
akiteta na waandishi na wafanyakazi wa Benki ya Exim kabla ya kukabidhi
cheti cha kimataifa cha ubora wa viwango cha ISO kwa kituo cha mafunzo
cha benki hiyo. Akishuhudia wapili kushoto ni Mkuu wa kitengo cha
kudhibiti Majanga wa Benki ya Exim David Lusala.
Na Mwandishi Wetu
KITUO
cha mafunzo cha Benki ya Exim ya Tanzania maarufu kama ‘Exim Academy’
kimetunukiwa cheti cha kimataifa cha ubora wa viwango (ISO 9001:2008)
ikiashiria ubora wa mafunzo yatolewayo na kituo hicho.
Kituo
hicho kilizinduliwa na benki hiyo mwaka jana kwa lengo la kuongeza
ufanisi na uwezo kwa wafanyakazi na tayari kinatoa programu muhimu za
kibenki kwa wafanyakazi wa benki hiyo.
Akizungumza
na waandishi wa habari wakati wa kupokea cheti hicho jijini Dar es
Salaam mwishoni mwa wiki, Afisa Fedha Mkuu wa benki hiyo, Bw. Selemani
Amani alisema cheti hicho kitakua chachu ya ubora na ufanisi wa huduma
zilotololewazo na benki hiyo.
“Tunayofuraha
kupata utambulisho huu wa kimataifa. Sasa tumeanza kuona kuwa jitihada
za benki yetu za kutoa huduma zinazotambulika kimataifa na zenye viwango
vya kukidhi matakwa ya wateja wetu ” alisema.
Alisisitiza
kuwa cheti hicho kimepatikana kwa muda muafaka hasa benki hiyo ikiwa
kwenye utekelezaji wa mpangop kabambe wa uboreshaji kazi na utoaji
huduma kwa wateja kwa ujumla.
“Mkakati
uliouanzisha na benki yetu miaka michache iliyopita sasa umeanza kuzaa
matunda baada ya benki yetu kuibuka mshindi wa jumla katika kipengele
cha huduma kwa wateja mwaka jana kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na
kampuni ya ukaguzi wa hesabu ya kimataifa ya KPMG iliyotafiti benki 32
nchini Tanzania.
“Mafanikio
yasingepatikana bila utendaji mzuri wa wafanyakazi wetu kwa ujumla.
Hatutabweteka na mafanikio hayo. Tutaendelea kuwekeza katika utoaji
huduma bora kwa wateja wetu vizuri zaidi siku za usoni, ” aliongeza.
Naye
Mwaklishi wa Kampuni ya ACM Tanzania Tawanda Manyuchi, kampuni ya
kitanzania iliyopewa dhamana na kampuni ya kimataifa ya Uingereza
ijulikanayo kama United Kingdom Accreditation Service (UKA) kufanya
tathmini ya mifumo ya uongozi wa chuo hicho cha mafunzo cha benki hiyo
wakati wa hafla hiyo alisema cheti hicho ni cha kwanza kutolewa kwa chou
cha mafunzo kwenye taasisi za kifedha, si kwa Tanzania pekee bali pia
na Afrika Mashariki kwa ujumla.
“Kufikia
viwango hivyo vya kimataifa inahitaji jitihada nyingi. Ni matumaini
yangu kuwa baada ya Benki ya Exim kupata cheti hiki sasa itawekeza nguvu
zake kupata viwango vya kimataifa kwenye idara zake zote,” Manyuchi
aliongeza.
0 comments:
Post a Comment