SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Monday, December 16, 2013

BREAKING NEWS: KIGOGO CCM AUAWA JIJINI MWANZA

Clement Mabina enzi za uhai wake.
Taarifa zilizotufikia ni kwamba, Mwenyekiti wa zamani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Mwanza, Clement Mabina, ameuawa mchana huu Kisesa, Mwanza baada ya kumpiga risasi raia mmoja na yeye kuuawa katika ugomvi wa mashamba!
HABARI NA  GLOBAL PUBLISHER

********* 
Aliyekuwa Mwenyekiti CCM wa mkoa wa Mwanza na Diwani wa Kata ya Kisesa, Mhe. Clement Mabina Auwawa na Wananchi Kwa Mawe
 Mwili wa Aliyekuwa Mwenyekiti CCM wa mkoa wa Mwanza na Diwani wa Kata ya Kisesa, Mhe. Clement Mabina baada ya kushambuliwa 

Mwili wa Aliyekuwa Mwenyekiti CCM wa mkoa wa Mwanza na Diwani wa Kata ya Kisesa, Mhe. Clement Mabina baada ya kufikishwa hospitali ya rufaa Bungando.

---
 Aliyekuwa Mwenyekiti CCM wa mkoa wa Mwanza na Diwani wa Kata ya Kisesa, Mhe. Clement Mabina  ameuwawa na wananchi wenye hasira kwa kupigwa na mawe na silaha za jadi mwendo wa saa saba mchana.

Imeelezwa kuwa sababu ya kumwuua Mabina inatokana na ugomvi wa ardhi ambapo kesi ya eneo hilo ilikuwa ikiendelea mahakamani, lakini mchana wa leo, marehemu Mabina alionekana akipanda miti na kuweka mawe ya msingi katika eneo lenye ugomvi na wananchi walipomhoji kuhusu kibali cha mahakama cha kufanya hivyo, inaripotiwa kuwa aliwatolea lugha chafu na kuwatisha kwa bunduki ambapo alifyatua risasi.

Inaripotiwa kuwa risasi moja ilimuua mwananchi na alipoishiwa risasi, wananchi walimvamia kwa silaha mbalimbali ikiwemo mawe na mapanga hadi kumsababishia mauti.
NA HAKI NGOWI

0 comments:

Post a Comment