Muonekano wa jukwaa kwa ajili ya kuangalia mechi kati ya Manchester United na Aston Villa katika viwanja vya Coco Beach jana. Waliopo stejini ni washereheshaji Adamu John na Khamisi Saidi. Droo ya moja kwa moja (live) ya kuwatafuta na kuwatangaza washindi wa tiketi mbili za kwenda Old Trafford itachezwa jana
Kundi la kucheza la Vinoko likionesha manjonjo yao kabla ya shoo ya jana ambapo watafanya shoo pamoja na wasanii wengine wa Bongo Fleva.
Kundi la kucheza la Vinoko likionesha manjonjo yao kabla ya shoo ya jana ambapo watafanya shoo pamoja na wasanii wengine wa Bongo Fleva.
Mchezaji wa zamani wa timu ya Manchester United, Andy Cole akiwa ndani ya Bongo.
Mchezaji wa zamani wa timu ya Manchester United, Andy Cole yupo nchini kwa udhamini mkubwa wa kampuni ya mitandao ya simu za mkononi ya Airtel kupitia promosheni yake ya Mimi ni Bingwa.
Mchezaji huyo leo atakuwepo kwenye viwanja vya Coco beach ambapo ataweza kujumuika na wananchi mbalimbali kwa ajili ya kushuhudia moja kwa moja mechi kati ya Manchester United na Aston Villa.
Cole pia atahudhuria droo ya moja kwa moja (live) ya kuwatafuta na kuwatangaza mshindi wa tiketi mbili za kwenda Old Trafford, kabla ya kuungana na mashabiki wa Man United kuangalia mechi moja kwa moja (live) itakayoonyeshwa Coco beach kati ya Manchester United na Aston Villa itakayochezwa Jumapili.
Akizungumza na waandishi wa habari janajijini Dar es Salaam, Cole alisema atakuwa mwenye furaha kukutana na baadhi ya mashabiki wake na pia kushuhudia moja kwa moja mechi hiyo pamoja nao.
“Nitakuwa mwenye furaha sana kukutana na mashabiki wa mpira wa miguu, nitafurahia kukutana na wote ambao wanajali mchezo huu na pia nitafurahi kushuhudia droo hii ya kumpata mshindi wa tatu wa tiketi ya kuja Old trafford” alisema Cole.
Tayari jukwaa kwa ajili ya kushuhudia mchuano mkali kati ya Manchester United na Aston Villa limeshaandaliwa katika viwanja hivyo.
Ziara hiyo ya Andy Cole nchini ina lengo la kuwapatia uzoefu washindi wa tiketi za promosheni ya Airtel ya 'Mimi ni Bingwa' ambao watasafiri kwenda kuangalia mechi za klabu ya Manchester United moja kwa moja (live) katika uwanja wa Old Trafford.
Hii ni ziara ya pili Tanzania kwa mchezaji Cole baada ya kutembelea Tanzania mwaka 2011 alipozindua mpango wa kutafuta vipaji wa Airtel Rising Star.
0 comments:
Post a Comment