Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisalimiana na baadhi ya wananchi wa Wilaya ya Moshi Vijijini, mara
baada ya kuwasili kwenye Kituo cha kusambaza umeme cha Makuyuni Wilaya
ya Moshi Vijijini Tarafa ya Himo Mkoa wa Kilimanjaro leo kwa ajili ya
kuzindua rasmi miradi ya ukarabati wa Vituo vya Kupoza Umeme na Ujenzi
wa Njia ya kusafirisha Umeme katika Mkoa wa Kilimanjaro.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akifunua kitambaa ikiwa ni ishara ya kuweka Jiwe la msingi, katika
uzinduzi rasmi Miradi ya ukarabati wa Vituo vya Kupoza Umeme na Ujenzi
wa Njia ya kusafirisha Umeme katika Mkoa wa Kilimanjaro. Hafla hiyo ya
uzinduzi imefanyika leo, Oktoba 7, 2013 katika Kituo cha kupoza umeme
cha Makuyuni Wilaya ya Moshi Vijijini Tarafa ya Himo Mkoa wa
Kilimanjaro. Kulia ni Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter
Muhongo na nyuma yao ni Balozi wa Japan nchini, Masaki Okada.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akikata utepe ikiwa ni ishara ya kuzindua rasmi Miradi ya ukarabati wa
Vituo vya Kupoza Umeme na Ujenzi wa Njia ya kusafirisha Umeme katika
Mkoa wa Kilimanjaro. Hafla hiyo ya uzinduzi imefanyika leo, Oktoba 7,
2013 katika Kituo cha kupoza umeme cha Makuyuni Wilaya ya Moshi Vijijini
Tarafa ya Himo Mkoa wa Kilimanjaro. Kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi
wa Tanesco, Felician Mramba, Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter
Muhongo (kushoto kwa Makamu) ni Balozi wa Japan nchini, Masaki Okada na
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal
na baadhi ya viongozi wakitembelea kukagua mitambi ya kusambaza umeme ya
Kiyungi.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisikiliza maelezo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Tanesco, Felician
Mramba, wakati alipotembelea kukagua Kituo cha kusambaza Umeme cha
Kiyungi, mkoani Kilimanjaro.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiangalia moja ya mtambo wa kisasa wa kusambaza umeme uliopo katika
kituo cha Makuyuni Wilaya ya Moshi Vijijini Tarafa ya Himo Mkoa wa
Kilimanjaro, wakati alipofika kituoni hapo kuzindua rasmi Miradi ya
ukarabati wa Vituo vya Kupoza Umeme na Ujenzi wa Njia ya kusafirisha
Umeme katika Mkoa wa Kilimanjaro, leo.
Mkuu
wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas gama, akizungumza kabla ya
kumkaribisha Waziri wa Nishati na Madidi, Prof. Muhongo, aliyemkaribisha
Makamu wa Rais, kuzingumza.
Picha ya pamoja baada ya uzinduzi huo.
Picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Tanesco baada ya uzinduzi huo.
Sehemu ya wananchi waliojitokeza kushuhudia uzinduzi huo.
Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais
0 comments:
Post a Comment