SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Thursday, October 31, 2013

Mahakama ya rufaa imeanza kupitia hukumu ya mwanamuziki maarufu nchini mwenye asili ya jamhuri ya kidemokrasia ya congo DRC Nguza Viking maarufu kama Babu seya na mwanawe Johnson Nguza maarufu kama Papii kocha.

 
  Nguza Vicking 'Babu Seya' akiwa na Mwanawe Johnson  Nguza au Papii wakiwa katika chumba cha Mahakama ya Rufaa Tanzania kabla ya kuanza kwa kusikilizwa kwa rufaa yao ya kuitaka mahakama hiyo kupitia upya hukumu iliyotolewa Februari 10-2010 na mahakama hiyo
  Nguza Vicking 'Babu Seya' akiwa na Mwanawe Johnson  Nguza au Papii wakiwa katika chumba cha Mahakama ya Rufaa Tanzania jijini Dar es Salaam jana, kabla ya kuanza kwa kusikilizwa kwa rufaa yao ya kuitaka mahakama hiyo kupitia upya hukumu iliyotolewa Februari 10-2010 na mahakama hiyo. Nguza na Papii walihukumiwa kifungo cha maisha jela baada ya kupatikana na hatia ya ubakaji na ulawiti.
 Nguza Vicking 'Babu Seya' akiwa na Mwanawe Johnson  Nguza wakiteta jambo na wakili wao, Mabere Marando.
  Watu waliohudhuria mahakama hapo wakifuatilia kesi hiyo.


 Nguza Vicking 'Babu Seya' akiwa na Mwanawe Johnson  Nguza 'Papii' wakiwa na nyuso za furaha wakati wakitoka katika Mahakama ya Rufaa baada ya majaji wa Mahakama ya Rufaa Tanzania kusikiliza maombi yao ya kuitaka mahakama hiyo kupitia hukumu iliyoitoa mwaka 2010.

  Johnson  Nguza 'Papii' akibusu mkono wake baada ya kuibusu ardhi mara baada ya kutoka mahakamani.

 Waandishi wa habari wakiwa chini wakati wa harakani za kuchukua matukio mahakamani.Picha Zote na Francis Dande 
-----
Mwanamuziki Nguza Viking maarufu kama Babu Seya na wanawe kupitia Wakili Mabere Marando wameiomba Mahakama ya Rufaa, ifanye marejeo kuhusu hukumu iliyoitoa na ifute ushahidi uliowatia hatiani na adhabu ya kifungo cha maisha jela wanayoitumikia.
Marando aliliwasilisha ombi hilo, kwa takribani saa 2 mbele ya jopo la majaji watatu wa mahakama hiyo .

Jopo hilo linaongozwa na Jaji Nathalia Kimaro, akisaidiana na Jaji Mbarouk Mbarouk na Jaji Salum Massati.Wakili huyo alisema wateja wake wanaoomba mahakama ifute ushahidi uliowatia hatiani washtakiwa na badala yake iwaachie huru.Kwa habari zaidi bofya na Endelea.......

0 comments:

Post a Comment