SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Thursday, October 31, 2013

Tamasha la Mercedez Benz African Fashion Week lafana sana mjini Pretoria, Afrika Kusini

Mbunifu wa mavazi wa Kimataifa wa nchini Afrika ya Kusini, David Tlale akiwa na Mwanamitindo wa Kimataifa kutoka nchini Tanzania,Millen Magesa wakipita stejini mara baada ya kuonyesha mavazi yake katika tamasha la Mercedez Benz African Fashion Week lililofanyika kwenye Stesheni ya Treni ya Rovos, Mjini Tshwane,Pretoria nchini Afrika Kusini
Mwanamitindo wa Kimataifa kutoka nchini Tanzania,Millen Magesa akipita Stejini kuonyesha mavazi yaliyobuniwa na Mbunifu wa mavazi wa Kimataifa wa nchini Afrika ya Kusini, David Tlale wakati wa onyesho lililofanyika usiku wa kumamkia leo kwenye Stesheni ya Treni ya Rovos,Mjini Tshwane, Pretoria nchini Afrika Kusini.
 Wanamitindo mbali mbali wa nchini Afrika Kusini wakipita na mavazi ya aina mbali mbali stejini wakati wa tamasha la Mercedez Benz African Fashion Week.
 Wadau kutoka sehemu mbali mbali wakihudhulia tamasha la Mercedez Benz African Fashion Week. 
Chief Photographer wa Michuzi Media Group Othman Michuzi yupo huko kuleta vitu hivi

0 comments:

Post a Comment