SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Tuesday, June 4, 2013

SERIKALI imeendelea kuchukua hatua za kuhakikisha kuwa rasilimali za umma zinatumika kama zilivyokusudiwa kwa ustawi wa maendeleo ya nchi na wananchi wake.

Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa mbeya Ndugu Nicolausi Ntangu akifungua semina ya wadau wa ukaguzi wa ndani kanda ya nyanda za juu kusini iliyo fanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mkapa. jijini Mbeya
Mkaguzi wa Ndani wa Serikali Msaidizi Ndugu Chotto Sendo amesema semina hiyo ni sehemu ya mkakati wa Ofisi ya Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa serikali wa kuimalisha  mfumo wa uwajibikaji  na utawala bora katika matumizi  ya rasilimali za umma chini ya program ya maboresho ya usimamizi wa fedha za umma awamu ya nne( PFMRP IV).Wadau wa ukaguzi wa ndani kanda ya nyanda za juu kusini wakimsikiliza mgeni rasmi katika ufngunguzi wa warsha hiyo   Mkaguzi wa ndani wa wa serikali msaidzi kitengo cha mshahara bajeti Sanslaus Mpembe akimshukuru mgeni rasmi kwa ufunguzi wa semina hiyo

Afisa habari Alexander Lweikila akifafanua jambo wa wadau 
Picha ya pamoja
SERIKALI  imeendelea kuchukua hatua za kuhakikisha kuwa rasilimali za umma zinatumika kama zilivyokusudiwa kwa ustawi wa maendeleo ya nchi na wananchi wake.
Picha Na Habari Kwa Hisani Ya Mbeya Yetu.

0 comments:

Post a Comment