SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Thursday, June 6, 2013

R. I.P ALBERT MANGWEA, AZIKWA RASMI NYUMBANI KWAO MJINI MOROGORO


Wakazi wa mjini Morogoro wakibeba Jeneza lenye mwili wa marehemu Albert Mangwe, kushusha makaburini tayari kwa kuzikwa leo mchana.
Kabla ya kuzikwa, wananchi wa Morogoro walipata fursa ya kuuaga mwili huo kwenye uwanja wa Jamhuri, ambapo Umati mkubwa wa wananchi ulijitokeza kutoa heshima zao za mwisho kwa mwili wa Ngwair aliyefariki nchini Afrika Kusini, Mei 28. Wasanii wengi kutoka Dar es Salaam nao wamehudhuria maziko hayo.
Mwili wa Mangwea ukihifadhiwa kwenye nyumba yake ya milele enel ya Kihonda Morogoro karibu kabisa na kaburi la baba yake mzazi.
Sehemu ya umati wa watu waliohudhuria maziko hayo
Umati wa watu ukishuhudia maziko hayo....
Picha Kwa Hisani Ya Mafoto

0 comments:

Post a Comment