Waandishi wa habari na wanaharakati wakimsubiri kumpokea Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Absalom Kibanda.
Waandishi wa habari na wanaharakati wakisubiri kumpokezi ya Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Absalom Kibanda.
Umati wa waandishi wa habari pamoja na wanaharakati wakiwa katika mapokezi ya Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri.
Baadhi ya wapiga picha wakiwa Uwanja wa Ndege wakati wa mapokezi ya Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Absalom kibanda.
Waandishi wa habari na wanaharakati wakimsubiri kumpokea Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Absalom Kibanda.
Mjumbe wa Bodi wa Jukwaa la wahariri, Theophil Makunga akimlaki Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Absalom Kibanda alipowasili jana kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere akitokea Afrika Kusini kwa matibabu.
Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya New Habari 2006 Ltd, Absolom Kibanda, akiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere,jana mchana. Hapa akiina na kuanza kulia baada ya kuonana na sura za watu wake wa karibu.
Kibanda akihojiwa na wanahabari baada ya kuwasili.
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF), Absalom Kibanda akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam jana.
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF), Absalom Kibanda akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam Jana
Kibanda akiwasili jana.
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF), Absalom Kibanda akitokwa na machozi muda mfupi baada yakuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam Jana.Picha na Mdau Mroki Mroki na Muhidini Sufiani
---
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Absalom Kibanda amerejea chini jana kutoka Afrika Kusini alikokuwa akitibiwa na kusisitiza kwamba hatanyamaza kuzungumzia janga la kushambuliwa kwake.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, Dar es Salaam, Kibanda alisema asingependa kuona jambo hilo linamtokea mwandishi mwingine wa habari.
Kibanda, ambaye pia ni Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya New Habari (2006) Ltd, alikuwa akitibiwa huko baada ya kushambuliwa na kuumizwa vibaya na watu wasiofahamika usiku wa Machi 5, mwaka huu.Alisema kutokana na hali hiyo, waandishi wanapaswa kuwa na mshikamano ili kuhakikisha matukio ya aina hiyo hayajirudii.
“Waandishi wana nafasi kubwa ya kuliondoa taifa katika hali hii. Waendelee kuandika na kuelimisha wananchi ili nao wasaidie kuzuia ukatili wa aina hii. Hatuwezi kuishi katika nchi ambayo watu wanafanyiwa ukatili mkubwa kiasi hiki halafu wanaachwa hivihivi,” alisema Kibanda.Kwa habari zaidi Bofya na Endelea.........
0 comments:
Post a Comment