Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Irene Kasyanju akimkaribisha Katibu Mtendaji wa Bodi ya Ushauri kuhusu Masuala ya Rushwa ya Umoja wa Afrika (African Union Advisory Board on Corruption-AUABC), Prof. Adolphe Lawson mara baada ya kuwasili Wizarani kwa ajili ya mazungumzo kuhusu mpango wa kuanzishwa kwa Makao Makuu ya AUABC Mkoani Arusha, Tanzania. Mazungumzo hayo yalifanyika Wizarani tarehe 19 Aprili, 2013.
Prof. Lawson akimweleza jambo Balozi Kasyanju wakati wa mazungumzo yao.
Balozi Irene Kasyanju akiwa katika mazungumzo na Prof. Lawson.
Prof. Lawson (kushoto) akiendelea na mazungumzo na Balozi Kasyanju huku Bw. Benedict Msuya (kulia), Afisa Mambo ya Nje katika Kitengo cha Sheria akinukuu mazungumzo hayo.
Picha na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
0 comments:
Post a Comment