SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Tuesday, April 9, 2013

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AENDESHA HARAMBEE YA MFUKO WA UDHAMINI WA ELIMU YA JUU WA MWALIMU NYERERE

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake
 Makamu wa Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akionyesha moja ya Sarafu iliyopigwa mnada katika harambee ya Mfuko wa Udhamini wa Elimu ya Juu wa Mwalimu Nyerere, iliyofanyika jana Aprili 8, 2013 katika Ukumbi wa Benki Kuu (BOT) jijini Dar es Salaam, ambayo ilinunuliwa na Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Reginard Mengi kwa Sh. milioni 20. Kushoto ni Waziri wa Fedha Dkt. William Mgimwa. Harambee hiyo ilifanyika jana April 8, 2013 katika Ukumbi wa BOT.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Reginard Mengi, baada ya kununua sarafu kwa Sh. milioni 20, wakati wa Harambee ya Mfuko wa Udhamini wa Elimu ya Juu wa Mwalimu Nyerere, iliyofanyika jana April 8, 2013 katika Ukumbi wa Benki Kuu (BOT) jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa harambee hiyo.Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais

0 comments:

Post a Comment