SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Wednesday, April 10, 2013

Breaking News...

Maradhi Temeke Kwaheri…..
“John. Nakupa silaha hizi zenye thamani kubwa sana kama unavyoona, sasa naamini kuwa sitosikia tena wakazi wa Temeke wakilalamika eti bado maradhi yanawasumbua. Huwa natembea sana Temeke na ningependa nikikatiza mitaa ile nikutane na watu wenye siha njema na nyuso zenye bashasha. Sijui kama umenielewa John?” alimalizia nami sikuwa na jibu lingine zaidi ya “Nimekuelewa mzee. Nitajitahidi”
Ndiyo. Niliitikia hivyo kwa furaha na tabasamu usoni kwa kuwa nilikuwa najua ubora wa silaha nilizokabidhiwa hazikuwa na msalie mtume kwenye kufagia “kijiji cha maradhi” yoyote sugu! Nikajisemea sasa maradhi Temeke yamekalia kuti kavu. Lakini, huyu Ben Mahenya ni nani? Ndugu Msomaji huyu ndiye mmiliki wa gazeti hili unalonisoma hapa, lakini Mungu ana mambo mengi sana maana nikikuambia kuwa ndiye pia muagizaji wa dawalishe hizi niziitazo “silaha” toka Afrika ya kusini utadhani kuwa huyu ni mtu mzee ambaye ana busara sana kwa kuwa sote tumezoea kuona wazee kuwa na busara zaidi na kujiridhisha kuwa busara ndio dira ya mzee yeyote katika maamuzi. 
Lakini huyu siye! Huwa nakutana naye mara kwa mara, na nakuhakikishia msomaji wangu kuwa huyu jamaa kwa akili zangu zote nimeshindwa kujua kama ni mzee, au kijana na kubaki na jibu moja tu kuwa Ben ni mjanja sana! Tuachane na Ben, Hebu tuangalie katika hii “arsenal” au ghala la silaha alilonokabidhi kuna nini?
Kama nilivyokuambia ndugu msomaji kuwa jamaa ni mjanja sana nilibaini kuwa mitishamba hii toka Afrika ya kusini kwanza kabisa imekuja na kipimo maarufu sana katika tiba duniani kiitwacho (BMI) yaani Body Mass Index ambacho kina uwezo mkubwa kubaini vyanzo vyote vya maradhi sugu mwilini mwa binadamu. Ni kipimo chenye uwezo wa kujua kama afya ipo sawa au la kabla hujasema unaumwa nini. Nilifurahi. Nikakipa kipimo hiki jina la “Binocular” maana bila hiki ingekuwa ngumu kuyafuata maradhi bila kujua utayaonaje. Lakini kama unaona kila ukitibiwa maradhi yanajirudia wewe njoo uone ninavyo yakomesha!
Nilipo funua mfuko mkubwa uliopo mbele yangu niliguna kwa furaha. Niliziona silaha kali sana ambazo sijaziona tena hapa nchini kwetu kabla “mjanja” huyu hajazileta. Zilikuwa mitishamba zenye akili ya kufagia “Kijiji” cha maradhi yoyote mwilini! Zilikuwa Go!Man, Go!Woman, Go!Focus na Go!Workout. Ndiyo. Kwa tafiti nilizofanya kupitia Rumours Africa ni kwamba toka niingize mitishamba hii maabara mwezi September’2012 Go! Ilionyesha ubabe sio tu wa kufagia maradhi niliyoshtakiwa na mgonjwa, bali baada ya matumizi ya mwezi mmoja mgonjwa alionekana ana siha njema kupita ile ya pundamilia na ngozi yake iling’ara kama mtoto wa nyoka aotaye jua asubuhi… Kifupi afya ilirudisha heshima na adabu za wagonjwa bila kupenda mpaka dawa hii nikaipa jina la AK47 kama ASANTE na SALUTI kwa kampuni inayotengeneza mitishamba hii – Nativa, South Africa.
Si dawa za kemikali, hapana. Ila zina sura ya dawa za hospitali toka boksi, kopo, mpaka vidonge ambavyo unakunywa viwili kila baada ya chain a baada ya mwezi tu badala ya kushukuru umepona, utabaki unashangaa kwa afya tele uliyoipata kupitia Go!Man au kama ni mwanamke kupitia Go!Woman. Kama ulikuwa na kisukari, presha, maumivu ya ajali na uzee, Hedhi inayosumbua, maradhi ya mara kwa mara, nguvu za uzazi magonjwa ya ngozi, kujaa gesi matumboni, maumivi ya mgongo na miguu kuvimba, na maradhi yoyote makubwa na madogo pia utakayosema nakuhakikishia kuwa nikikupa Go!Man/Woman pamoja na mitishamba sindikizaji uhakika wa kuyaaga maradhi uko mkononi mwako tu… Hata hivyo, gharama za vipimo, ushauri na dawa si ghali sana ukilinganisha na uhakika wa utakachopata. Inaweza kukugharimu shilingi elfu sitini kama si mgonjwa kupindukia mpaka laki nne kama hali ni mbaya lakini wapo pia wanaotumia pesa zaidi ya hapo ila uhakika ni kuwa kila kitu kinakuwa sawa kabisa. Wapo pia wanaosumbua akili zao kutwa ili wapate riziki zao. Wao tumewaletea Go!Focus kwa kutuliza ubongo sio umeze panadol zikalete vidonda tumboni. Na wale wanaosulubu miili kutwa kutafuta riziki zao nao wanayo Go!Workout ipo kwa ajili yao na si lazima kungoja mpaka uumwe ndio uitafute Go!Focus au Go!Workout, bali ndio itakufanya uzifurahie kazi zako siku zote na ufanisi uwe bora zaidi…
Hivyo Wanatemeke hii ni nafasi yenu ya kipekee kuja kupata tiba hizi asili toka afrika ya kusini tena kwa gharama nafuu sana. Unatakiwa ufike Polisi Post ya viwanja vya Mwembeyanga Temeke, pale utaona gereji kubwa tu imeandikwa KWADU MIKOMA ENTERPRISES GARAGE. Rumours Africa ipo ubavuni mwa jingo hilo na ofisi zinajulikana kama “Kwa Bondia” kwa kuwa nilipigana sana ngumi nimestaafu! Karibuni sana. Kulea maradhi ni ujinga lakini wagonjwa wa maeneo mengine tungewaomba wasubiri tuwahudumie Wanatemeke kwanza halafu tutahamisha kituo kwenda tena sehemu nyingine tukianzia na Kinondoni mjiandae….
Lakini, Nilipofunua chini ya mfuko huu wa silaha kali nilikuta pia mtishamba jeuri sana kwa wazee waliozidi miaka 50, watu wenye uzito mkubwa na mdogo, waliopatwa na ajali, waliofanyiwa upasuaji nk. Hawa wameletewa OsteoEze. OsteoEze ni mtishamba wenye vidonge 60 tu nao. Ukiuangalia kama dawa za dukani lakini sio! Niliwahi kumpa mzee aliyekunywa siku 16 tu akanipigia simu akisema amepona kabisaaa! Nilifurahi. Nikamwambia hizi dawa kwa umahiri wake wa kutibu nimedhamiria kuzipa majina. Na yeye kama shuhuda wa kwanza nimempa nafasi ya kuibatiza jina dawa hiyo. Yeye alinijibu hivi: “Nimefurahi sana kijana wangu. Dawa hii iitwe Shotgun kwa kuwa ndio bunduki yangu ninayoiamini hapa ndani lakini imeshindwa kufukuza maradhi haya!” Nilicheka sana, lakini nilipowaambia staff wa Rumours Africa wote walicheka na toka siku hiyo jina la dawa hiyo hapa kwetu ni hilo.
OsteoEze hutaiamini ukioona, lakini kama nilivyokuambia kuwa haya ni mambo ya mtu “mjanja” sana. Temeke nawaomba woote mnaojisikia mna maradhi hayasomeki katika viungo hasa ajali, uzee, mgongo, miguu, nyayo, au maumivu yoyote unayoona yanataka kukuzoea hayaponi wewe njoo utaona! Ukimaliza dozi hutalalamika tena. 
Mitishamba hii ambayo ni SILAHA zipo nyingi sana, tena Ben amenipa zaidi ya 120! Unaijua dawa ya kukusaidia kubeba mimba weye? Au hata mimba yenyewe haishiki? Mumeo anazo nguvu za kukusaidia naye au jogoo kafa? Au unajua kuwa mwanao anatakiwa apewe dawa AFAULU? Ndiyo! Zipo dawa za kusafisha watoto ubongo pia zote mitishamba. Unaijua komesha ya kisukari? Au una mgonjwa kalala hoi hujui anaumwa nini? Kifupi nimepewa rungu la kuangamiza maradhi Temeke na kama mtayafichua basi kazi yangu itakuwa rahisi sana. Shime Wanatemeke njooni tupimwe, tujulikane maradhi yetu halafu mtaona mitishamba ya kizulu inatania kama ya watanzania au la.
Karibuni “Kwa Bondia” Mwembeyanga Temeke jirani na gereji ya Kwadu Mikoma utapata huduma hizi za mitishamba toka Afrika Kusini inayotengenezwa na Nativa! Wiki ijayo nikiwa hai nitawaletea zile za ukimwi, kansa, na zile za maradhi kama figo, ini, moyo nk. Wote njoeni tumalize matatizo haya.
John Haule
0768 215 956
rumoursafrica@gmail.com. 
Itaendelea….

0 comments:

Post a Comment