SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Friday, April 12, 2013

Aliyekuwa Mhasibu katika Ofisi ya Wakala wa Mkemia Mkuu wa Serikali,Godfrey Mbwilo Apandishwea Kizimbani Kwa tuhuma za wizi wa Sh150 milioni katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu


Aliyekuwa Mhasibu katika ofisi ya Wakala wa Mkemia Mkuu wa Serikali, Godfrey Mbwilo (katikati) akiwa chini ya ulinzi wa askari polisi akipelekwa kizimbani kwa tuhuma za wizi wa Sh150 milioni katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam jana.Picha na Venance Nestory
. -- 
 Aliyekuwa mfanyakazi wa Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Godfrey Mbwilo amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na tuhuma za wizi wa Sh153 milioni.

 Akisoma hati ya mashtaka jana mbele ya Hakimu Mkazi, Augustina Mmbando, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Tumain Kweka alidai kuwa mshtakiwa huyo alisomewa mashtaka jana mbele ya Hakimu Mkazi Augustina Mmbando na Wakili wa Serikali Tumaini Kweka alidai kuwa mshtakiwa alifanya makosa hayo kinyume na sheria ya kanuni ya adhabu. 

Kweka alidai kuwa Agosti 2, 2011 katika ofisi za Mkemia Mkuu wa Serikali, akiwa mtumishi wa umma aliiba Sh40 milioni mali ya Serikali zilizofika kwake kulingana na nafasi yake ya ajira. 

 Katika shtaka la pili, Kweka alidai kuwa Septemba 5,mwaka huo katika ofisi hizo aliiba Sh45 milioni mali ya Serikali zilizofika kwake kulingana na nafasi yake ya ajira.
Kwa Habari Zaidi Bofya Hapa

0 comments:

Post a Comment