SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Monday, March 18, 2013

MKAZI WA SUMBAWANGA AJISHINDIA MILIONI TANO KUPITIA MAHELA PROMOSHENI‏

Meneja wa huduma za ziada wa Vodacom Tanzania, Benjamin Michael (kushoto) akimkabidhi hundi ya shilingi milioni moja mshindi wa promosheni ya MAHELA, Bi. Ailine Maro (kulia) mkazi wa Alinde Estate Mbweni-Boko. Anayeshuhudia katikati ni rafiki yake Agness Richard. Jumla ya shilingi milioni 251 bado zinaendelea kushindaniwa katika promosheni hiyo inayoendeshwa na Vodacom Tanzania.
Meneja wa huduma za ziada wa Vodacom Tanzania, Benjamin Michael (kushoto) akimkabidhi hundi ya shilingi milioni moja mshindi wa promosheni ya MAHELA, Bw. Rugemalira Igangas (kulia) mkazi wa Mikocheni jijini Dar es Salaam, katikati ni Meneja Mahusiano wa Vodacom, Bw. Matina Nkurlu. Bado shilingi milioni 251 zinaendelea kushindaniwa katika promosheni hiyo.
Mshindi wa promosheni ya MAHELA, Bw. Rugemalira Igangas (62) akiongea na baadhi ya waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya ushindi wake katika promosheni hiyo inayoendeshwa na Vodacom Tanzania.
Afisa wa michezo ya kubahatisha nchini, Bi. Chiku Saleh, katikati pamoja na Meneja huduma za ziada wa Vodacom Tanzania, Benjamin Michael wakidhibitisha jambo wakati wa kuchezesha droo ya MAHELA inayoendeshwa na Vodacom Tanzania, ambapo Rabeca Sangu mkazi wa Sumbawanga alijishindia shilingi milioni tano, kushoto ni Meneja Mawasiliano wa Vodacom, Bi. Rukia Mtingwa.

0 comments:

Post a Comment