SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Saturday, October 6, 2012

ABU HAMZA AWASILI NCHINI MAREKANI


Abu Hamza
Mhubiri wa Kiislamu mwenye msimamo mkali, Abu Hamza, na watu wengine wane wanaoshukiwa kuwa magaida, wanatarajiwa kufikishwa mahakamani 

Jumamosi nchini Marekani baada ya kusafirishwa kutoka Uingereza.
Juhudi zao zilizogharimu fedha nyingi, kupinga kupelekwa Marekani, zilimalizika Ijumaa mjini London baada ya mahakama makuu kutupilia mbali rufaa iliyowasilishwa na Bwana Hamza.
Washukiwa hao watano walisafirishwa kwa ndege punde baadaye kuelekea Marekani.
Abu Hamza anakabili mashtaka kadha, pamoja na njama ya kuanzisha kituo cha mafunzo ya kijeshi katika jimbo la Oregon, Marekani.
Yeye na washukiwa wawili watafikishwa mahakama ya New York, na wawili wengine watafanyiwa kesi Connecticut.

0 comments:

Post a Comment