Picha juu na Chini Wanafunzi wa shule mbalimbali za msingi na sekondari jijini Dar wakiwa wamebeba mfano wa Njiwa kuashiria Amani katika maadhimisho wakiandamana kuelekea ukumbi wa Karimjee katika maadhimisho ya Siku ya Amani Duniani Jana.
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dkt. Alberic Kacou akimkaribisha Mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya Amani Duniani aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Dkt. Asha-Rose Migiro.
Dkt. Asha-Rose Migiro akisalimiana na Balozi wa Nigeria nchini Tanzania Dr. Ishaya Nanjabu.
Dkt. Migiro akiteta jambo na Dkt. Kacou wakati Balozi wa Nigeria Dr. Nanjabu akizungumza na mmoja wa maafisa wa jeshi hapa nchini wakati wakisubiri maandamano ya Amani.
Dkt. Migiro sambamba na Dkt. Kacou wakielekea kupokea maandamano ya Wanafunzi wa Shule mbalimbali jijini Dar katika maadhimisho ya siku ya Amani Duniani.
Mgeni rasmi Dkt. Migiro (katikati), Dkt. Kacou pamoja na Balozi wa Nigeria nchini Dr. Nanjabu (kushoto) wakiwa wamebeba sanamu mfano wa ndege aina ya Njiwa ikiwa ni Ishara ya Amani.
Mgeni rasmi Dkt. Asha-Rose Migiro akiimba nyimbo za kuhamasisha Amani pamoja na washiriki wa maandamano ya siku Amani Duniani.
Afisa Habari kutoka kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa Stella Vuzo akitoa utambulisho wa meza kuu.Katikati ni Mgeni rasmi Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Dkt. Asha-Rose Migiro, Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Dkt. Alberic Kacou (wa pili kushoto), Mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la Right to Play Bw. Francis Rwiza (kulia), Balozi wa Nigeria nchini Tanzania Dr. Ishaya Nanjabu na Wa pili kulia ni Program Manager wa Global Network of Religions for Children (GNRC) Bi. Elizabeth Mwase.
Wanafunzi wa shule mbalimbali za jijini Dar wakati wa maadhimisho ya Siku ya Amani Duniani yenye Kauli mbiu "AMANI ENDELEVU KWA UENDELEVU WA MASIHA YA BAADAE".
Mmoja wa viongozi wa madhehebu ya Dini kutoka BAKWATA akitoa sala wakati w ufunguzi wa maadhimisho ya siku ya Amani Duniani jana jijini Dar es Salaam.
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa hapa nchini Dkt. Alberic Kacou akitoa hotuba wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Amani Duniani ambapo amerejea kusisitiza kauli ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki-Moon katika ujumbe wake wa amani mwaka huu.
Amesema katika Siku ya Kimataifa ya Amani, Umoja wa Mataifa unatoa wito wa kusitishwa kabisa kwa mapigano mahali mbalimbali duniani kwa kuwa mapigano ya silaha yanashambulia mihimili muhimu ya maendeleo endelevu.
Bw. Kacou pia ametumia fursa hiyo kulipongeza Bunge la Tanzania kwa dhima yake ya kuhamasisha Utawala Bora na kupiga vita ufisadi ili kuleta maendeleo ya taifa.
Mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya Amani Duniani aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Dkt. Asha-Rose Migiro akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Amani Duniani leo jijini Dar es Salaam, ambapo pamoja na mambo mengine amesema Tanzania itaendelea kuwa mfano wa jinsi demokrasi inavyofanya kazi katika ukanda wa Afrika Mashariki.
Aidha amesema mchakato unaoendelea wa mabadiliko ya katiba umewaweka wanaume na wanawake wa Tanzania katika nafasi ya kuamua kuhusu kuimarisha manufaa ya Kidemokrasia, kuimarisha utawala bora na haki za binadamu.
Pichani ni baadhi ya mabalozi wanaowakilisha nchi zao pamoja na maafisa wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini wakisiliza hotuba ya mgeni rasmi Dkt. Asha-Rose Migiro (hayupo pichani).
Baadhi ya wageni waalikwa wakiwamo wawakilishi kutoka Serikalini, Mabalozi na Viongozi kutoka Ofisi za Kibalozi na Wanafunzi kutoka shule mbalimbali za jijini Dar.
Mwanafunzi wa shule ya msingi Airwing Brenda Simon aliyeshiriki shindano la Insha ya Siku ya Amani Duniani.
Mshindi wa Insha wa maadhimisho ya siku ya Amani Duniani kutoka Shule ya Sekondari Kibasila akisoma Insha yake mbele ya wageni waalikwa hawapo pichani.
Mkurugenzi wa shirika lisilo la Kiserikali la Right to Play Bw. Francis Rwiza akimkabidhi cheti pamoja na zawadi mshindi wa Insha ya maadhimisho ya siku ya Amani Duniani mwanafunzi wa shule ya msingi Airwing Brenda Simon.
Wanafunzi kutoka shule ya msingi Buguruni Viziwi wakitoa burudani wakati wa sherehe za maadhimisho hayo.
Dkt. Asha R0se Migiro akiimba pamoja na wanafunzi wa shule mbalimbali za jijini Dar wakati akiondoka ukumbini hapo.
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa hapa nchini Dkt.Alberic Kacou akimsindikiza mgeni rasmi Dkt. Asha-Rose Migiro baada ya shereh za maadhimisho hayo.
Dkt. Asha-Rose Migiro akifanyiwa mahojiano na vyombo vya habari nchini.
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Tanzania Dkt. Alberic Kacou akiteta jambo na baadhi ya mabalozi waliohudhuria sherehe za maadhimisho ya siku ya Amani Duniani zilizofanyika katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.
Afisa Habari kutoka kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa Stella Vuzo (wa nne kushoto) pamoja na wadau wakifurahia sherehe za maadhimisho ya siku ya Amani Duniani.
---
Na.Mwandishi wetu
Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Dkt. Asha Rose Migiro amesema ili amani idumu nchini kuna ulazima wa raslimali za nchi zitumika kwa maendeleo.Migiro amesema amani iliyopo nchini ni ya kujivunia na inahitaji kutunzwa na kuheshimiwa. Amesema hayo wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Amani duniani iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Dkt. Migiro amesema ili amani idumu ni lazima iwepo mipango madhubuti ya kuhakikisha uchumi unakua kwa kila nchi na kuhakikisha kwamba raslimali za nchi zinatumika vizuri ili kuleta maendeleo.Maadhimisho hayo yalihudhuriwa na mabalozi na baadhi ya viongozi wa serikali na wabunge.
CREDIT TO HAKI NGOWI
CREDIT TO HAKI NGOWI
0 comments:
Post a Comment