SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Thursday, August 9, 2012

Maalim Seif Atembelea Wafanyabiashara wa Jua Kali Saateni Zanzibar.


Mfanyabiashara wa soko la Saateni Khamis Ali Mohd akitoa maelezo kwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad kuhusiana na hali ya kudorora kwa biashara katika soko hilo, wakati Maalim Seif alipotembelea eneo hilo jana.


Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akiulizia bei ya viatu, wakati alipofanya ziara ya kutembelea eneo la biashara la Saateni mjini Zanzibar.maaarufu kwa jina la jua kali.

Mfanyabiashara ya mitumba katika soko la Saateni akitoa maelezo kwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad alipotembelea eneo hilo jana.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akiangalia biashara ya mitumba, wakati alipofanya ziara ya kutembelea eneo la biashara la Saateni mjini Zanzibar.(Picha na OMKR)
**==**

Na Hassan Hamad (OMKR).

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad ameelezea umuhimu wa kutafutwa muwekezaji kwa ajili ya kulijenga na kuliendeleza soko la saateni, ili kuweka mazingira bora ya kibiashara katika soko hilo.

Amesema mazingira yaliyopo sasa hayaridhishi kutokana na kutokuwa na miundombinu imara, hali inayowafanya baadhi ya wafanyabiashara kufikia uamuzi wa kulihama soko hilo na kuelekea darajani, eneo ambalo haliruhusiwi kwa wafanyabiashara wadogowadogo.

Maalim Seif ametoa kauli hiyo leo alipofanya ziara ya kutembelea soko la Saateni kuangalia hali ya biashara inavyokwenda hasa katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhan.

0 comments:

Post a Comment