SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Thursday, February 2, 2012

Mamlaka ya Bandari Tanzania (THA) Yatoa Hati Kwa Taasisi Tano Kusaidia Kupunguza Msongamano Wa Makontena Katika Bandari Ya Dar es Salaam

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (THA), Ephraim Mgawe (kulia) akimkabidhi Rais wa Chama cha Mawakala wa Forodha Tanzania (TAFFA), Stephen Ngatunga hati ya makubaliano ya kusaidia kupunguza msongamano wa makontena katika bandari ya Dar es Salaam kwa kuyahamishia katika Bandari Kavu. Hafla hiyo ilifanyika eneo la Bandari hiyo jana, ambapo taasisi nyingine nne zilipata hati hizo.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya TICTS, Nathan Bissett akikabidhiwa hati ya makubaliano na Mkurugenzi Mkuu wa THA, Mgawe.
Naibu Kamishna wa Forodha na Ushuru wa Bidhaa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Patrick Kisaka (kushoto) akipokea hati hiyo.
Katibu Mkuu wa Mawakala wa Meli Tanzania (TASAA), Peter Kirigini (kushoto), akipokea hati
Meneja Mwendeshaji wa Kampuni ya Tanzania Road Haulage (1980) LTD, Ali Hussein Lilan akipokea hati hiyo kutoka kwa Mgawe.
Viongozi hao wakitiliana saini mkataba huo
Baadhi ya wageni waalikwa wakishuhudia makabidhiano hayo.
Picha Zote na Mdau Richard Mwaikenda

0 comments:

Post a Comment