SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Friday, January 20, 2012

Airtel yakabadhi kompyuta nne kwa Shule ya Sekondari Mlangarini Arumeru Arusha

Ofisa Uhusiano wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel, Jane Matinde akikambidhi sehemu ya msaada wa kompyuta nne kwa Mbunge wa Arumeru Magharibi na Naibu Waziri wa Ardhi , nyumba maendeleo na makazi, Bw. Goodluck Ole Medeye kwa ajili ya Shule ya Sekondari ya Mlangarini iliyoko Wilayani Arumeru Mkoani Arusha.
Ofisa Uhusiano wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel, Jane Matinde akimuelekeza jambo Mbunge wa Arumeru Magharibi na Naibu waziri wa Ardhi, nyumba maendeleo na makazi, Bw. Goodluck Ole Medeye baada ya kumkabidhi kompyuta nne kwa ajili ya Shule ya Sekondari ya Mlangarini iliyoko Wilayani Arumeru Mkoani Arusha na kushoto ni Diwani wa kata ya Mlangarini, Bw.Mathias Erasto akishuhudia tukio hilo.

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Mlangarini iliyoko Wilayani Arumeru Mkoani Arusha, Bw. Elisa John Pallangyo akitoa maneno ya shukrani kwa kampuni ya simu ya Airtel kwa msaada mkubwa walioutoa kwa ajili ya shule hiyo, pichani kati ni mgeni rasmi wa tukio hilo, Mbunge wa Arumeru Magharibi na Naibu Waziri wa Ardhi, nyumba maendeleo na makazi, Bw. Goodluck Ole Medeye, sambamba na Diwani wa kata ya Mlangarini, Bw.Mathias Erasto akishuhudia tukio hilo na kushoto ni Ofisa Uhusiano wa Airtel.
========
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imetoa kompyuta nne kwa shule
ya sekondari Mlangarini iliyoko wilayani Arumeru Mkoani Arusha ikiwa
ni moja wapo kati ya shughuli za kutoa huduma zinazofanywa na kampuni
hiyo kwa jamii huku lengo hasa likiwa ni kukuza sekta ya elimu nchini.

Akizungumza kwa niaba ya kampuni ya simu za mkononi ya Airtel, Afisa
Uhusiano wa Airtel, Jane Matinde alisema, Airtel inajisikia faraja
kutembelea shule ya Mlagarini na kuwapatia kompyuta zitakazowawezesha
kupata vitabu mbalimbali kwa njia ya mtandao na kutoa fulsa kwa
wanafunzi wa sekondari kujifunza kutumia kompyuta wakiwa bado
mashuleni. Aidha aliahidi kuwa Airtel itaendelea kushirikiana na
serikali kupitia wizara ya elimu katika kuhakikisha elimu mashuleni
inaboreshwa.
Akiongea baada ya kukabidhiwa kompyuta hizo, Mbunge wa Arumeru
Magharibi na Naibu waziri wa Ardhi Nyuma Maendeleo na Makazi, Bw.
Goodluck Ole Medeye alisema, "tunashukuru sana kampuni ya simu za
mkononi ya Airtel kwa kuipatia Shule ya Sekondari Mlangarini kompyuta
zitakazowawezesha kupata habari na vitabu mbalimbali kwa njia ya
mtandao, kompyuta hizi zitarahisisha sana upatikanaji wa nyezo muhimu
za elimu kwa wanafunzi na walimu kwa kupitia mtandao.
Pia aliwaasa wanafunzi wa Mlangarini kutumia fulsa hiyo kujifunza na
si kutumia kompyuta hizo kuangalia mambo yasiyofaa katika internet, Ole
Madeye aliendelea kuwaasa na kuwapa changamoto wanafunzi kuweza
kupanua akili na kuwa wavumbuzi wa vifaa muhimu vitakavyosaidia
jamii kama ilivyovumbuliwa kompyuta.
Pamoja na haya alifafanua kuwa kompyuta hizo zitatumika pia kwa wakazi
wa maeneo hayo kwani makitaba ya wilaya itakuwa hapa shuleni hivyo
basi wakazi wa wilaya ya Arumeru watapata fulsa ya kutangaza biashara
zao kwa kupitia mtandao na kuweza kupata taarifa muhimu zitakazo
wasaidia katika kuboresha biashara zao na shughuli muhimu za wilayani
hapo pia aliongeza Madeye.
Naye Diwani wa kata ya Arumeru, Bw Mathias Manga alichukua fulsa pia
kuwashukuru kampuni ya simu za mkononi ya Airtel na kuwaasa wanafunzi
kutumia kompyuta hizo vizuri na kuzitunza ili zisaidie wanafunzi wengi
zaidi shuleni hapo. Aliwaasa wanafunzi hao kuchukua nafasi hii ya pekee
kujifunza na kutumia kompyuta hizo katika kujijenga kielimu na
kitaaluma zaidi.
Akitoa shukrani, mwalimu mkuu wa shule, Elisa John Pallangyo
ameipongeza Airtel kwa kuwafikishia msaada muhimu shuleni hapo na
kuahidi kwa kupitia msaada kiwango cha elimu shuleni hapa kitapanda
kwani changamoto mbalimbali walizokuwa nazo kama vile internet,
upatikanaji wa nyenzo muhimu katika kufundishia zitapungua kwa kiasi
kikubwa sana.
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imekuwa ikitoa misaada mbalimbali
kama vile Vitabu vya shule ya sekondari, kuchangia katika huduma za
afya ambapo wiki iliyopita waligawa baiskeli kumi katika vituo vya
afya wilayani Misungwi na kutoa mchango wao pia katika sekta ya
michezo kwa kudhamini michezo mbalimbali nchini.

0 comments:

Post a Comment