SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Friday, January 20, 2012

KIKONGWE MBAKAJI AFIKISHWA MAHAKAMANI - MBEYA

Kikongwe huyu Asangwile Kihaka miaka 78 ndiye anayetuhumiwa kubaka mwanafunzi wa miaka 12 anayesoma shule ya msingi mbata jijini mbeya.
Baba mzazi wa binti aliyebakwa na Mzee Asangile Kihaka (70), anayefahamika kwa jina la Bwana Ekson Nazareth (47), ambaye pia ni mzee wa baraza mahakama ya Mwanzo ya Mbeya Mjini..

Mmoja wa wananchi wa eneo la Ghana akilaani vikali kitendo cha Mzee Asangile Kihaka (78) kumbaka binti wa miaka 12, mwanafunzi wa darasa la 7 katika Shule ya Msingi Mbata, ambapo ni tukio la tatu la mzee huyo kutenda.
======
Habari na mwandishi wetu.
Mzee Asangile Kihaka mwenye umri wa miaka 75 mkazi Ghana amefikishwa katika mahakamani ya hakimu mkazi mkoa wa Mbeya jana akituhumiwa kumbaka mtoto wa miaka 12 disemba 14 mwaka jana.


Akisoma shtaka linalomkabili mzee huyo mwanasheria wa Serikali Roda Ngole mbele ya hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo Zabibu Mpangule amesema mzee Asangile alitenda kosa hilo akiwa nyumbani kwake baada ya kumrubuni mtoto huyo kumpelekea kuni nyumbani kwake na baada ya mtoto kufika ndani mzee huyo alianza kumwingilia kimwili kwa nguvu.


Amesema kitendo hicho ni kinyume cha kifungo cha Sheria 130 sura ya pili E na kifungu namba 131 sehemu ya kwanza sura ya 16 marekebisho ya mwaka 2002.


Hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo Zainabu Mpangule ameihairisha kesi hiyo hadi February mosi mwaka huu na kwamba mtuhumiwa amerudishwa rumande baada ya kukosa dhamana ya shilingi laki tano.
Chanzo: Bofya

0 comments:

Post a Comment