SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Friday, December 2, 2011

Mchekeshaji Vengu Azushiwa Kifo

Uvumi ulioenea katika jamii kuwa Msanii wa Maigizo na vichekesho Joseph Shamba almaarufu  Vengu amefariki dunia si wa kweli na umekanushwa vikali.
Kwa mujibu wa mmoja wa wasanii wa kundi hilo la Ze Original Komedi, ambaye hata hivyo hakupenda kutaja jina lake kwani si msemaji halali wa Kundi hilo na kunitaka Niwasiliane na Sekion David juu ya taarifa kamili ya msanii huyo.
“Achaneni na uzushi huo..mshikaji bado yupo hai na Mungu anazidi mpigania na hali yake hivi sasa inaendelea vyema,” alisema msanii huyo.
Aidha Seki alipotafutwa alidai kuwa Vengu ni mzima na anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alikolazwa.
Seki pia alibainisha kuwa hivi sasa suala la kuzungumzia afya ya Vengu kiundani lipo kwa wanafamilia isipokuwa wao wanajua Vengu bado mzima.
Juhudi za blogu hii ya watu kumpata msemaji wa familia ambaye ni baba Mzazi wa Vengu, Mzee Shamba zinaendelea ili kuutabanaisha umma juu ya afya ya msanii huyo kipenzi cha watanzania hasa kutokana na umahiri wake wa kuiga sauti za viongozi hasa Augustino Mrema.
Chanzo:  FATHER KIDEVU

0 comments:

Post a Comment