SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Tuesday, December 6, 2011

Maelfu wamzika Mr Ebbo

Maelfu ya wakazi wa mji wa Arusha jana waliungana na wanafamilia wa Msanii Maarufu Mr Ebbo katika misa maalum ya kuuombea Mwili wa Marehemu motto wao na baade katika maziko yaliyofanyika mjini humo.
Miongoni mwa viongozi walioshiriki mazishi hayo ni pamoja na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Goodluck Ole Medeye ambaye ni Mbunge wa Arumeru Mashariki pamoja na Waziri wa Zamani wa Mazingira katika Ofisi ya Makamu wa Rais, Dk. Batilda Buriani na wasanii mbalimbali wa muziki nchini.
Mr Ebbo alifariki mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya kuugua kwa muda.
Askofu akiongoza misa ya kumuombea Marehemu Abel Loshilaa Motika "Mr Ebbo" nyumbani kwao mjini Arusha jana .
Familia ya marehemu Ebo katikati mama mzazi,kulia baba yake mzazi na kaka yake mkubwa Olais Motika wakiwa msibani hapo.
Ndugu mbalimbali wakiaga mwili wa marehemu.
Wazazi wa Mr Ebbo wakiwa na Mbunge wa Zamani na Waziri wa Mazingira, Dk. Batilda Buriani.
Watoto watatu wa marehemu Mr Ebo ,wakifarijiwa na ndugu.
Naibu waziri wa Ardhi ,nyumba na makazi,Goodluck Ole Medeye kulia akimfariji baba mzazi wa marehemu Ebo,mzee Loshilaa Motika katika ibada ya mazishi ya marehemu Mr,Ebbo juzi nyumbani kwake Moshono ,katikati ni aliyewahi kuwa waziri wa mazingira dkt Batilda Buriani.
Kaka mkubwa wa marehemu mr,Ebbo Olais Motika kushoto na mdogo wake wa mwisho Jackson Motika,wakiwa katika ibada ya mazishi ya marehemu,Mr Ebbo jana nyumbani kwao Moshoni jijini Arusha.
Maelfu ya wakazi wa mjini Arusha wakiwa katika foleni ya kwenda kutoa heshima za mwisho kwenye mwili wa Marehemu Mr Ebbo.
Na mrokim blogspot

0 comments:

Post a Comment