SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Saturday, July 2, 2011

KIJANA PASCAL ANAOMBA MSAADA WA MATIBABU YA KUONDOLEWA MFUPA WA ZIADA KATIKA MGUU WAKE WA KULIA

Kijana Pascal
Hii ni Sehemu inayoonyesha mfupa huo wa ziada unaoendelea kukua na kumsababishia maumivu makali. 
Kijana Pascal Issa mkazi wa Tegeta jijini Dar es Salaam ameomba msaada wa fedha au matibabu kwa ajili ya upasuaji wa mguu wake wa kulia wenye mifupa miwili, Kijana huyo aliyefika katika Ofisi za MO BLOG  jijini Dar es Salaam.
Aidha Kijana huyo amewaomba wasamaria wema kumsaidia ili aondokane na mateso anayoyapata hususani wakati wa usiku ambapo mfupa huo wa ziada ulioanza kujitokeza tangu akiwa na umri miaka 7 mpaka sasa akiwa na miaka 24 kuendelea kukua bila matumaini ya kupata matibabu.
Kwa yoyote atakayeguswa na tatizo la kijana huyo awasiliane naye kwa namba             +255657069870       au awasiliane na Meneja wa MO BLOG kwa namba             +255714940992       kwa ajili ya mawasiliano zaidi.
MO BLOG inawaomba wadau wanaoweza kumsaidia hata kupata Daktari wa kumtibu kwani kutoa ni moyo na hujafa hujaumbika.

0 comments:

Post a Comment