SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Sunday, June 12, 2011

MAADHIMISHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA NA UMOJA WA MATAIFA NA AFRIKA KUFANYIKA JUNI 20 HADI 23!!


Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Rasilimali watu Ofisi ya Rais Menejimenti  ya Utumishi wa Umma Dk. Faisal Issa (Kushoto) akijibu swali la muandishi wa Habari (hayupo pichani) kuhusu wajibu wa mtumishi wa Umma kwa jamii kulia ni Mathias Kabunduguru ambaye ni Mkurugenzi wa Sera. Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa mikutano uliopo makao makuu ya ofisi hizo zilizopo jijini Dar es Salaam.
Msemaji wa  Ofisi ya Rais Menejimenti  ya Utumishi wa Umma Zamaradi Kawawa (kulia) akimkaribisha Naibu katibu Mkuu wa ofisi hiyo HAB Mkwizu (kushoto) ili aweze kuzungumza na waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu maadhimisho ya siku ya utumishi wa Umma ya Umoja wa Mataifa na Afrika ambayo itafanyika kuanzia tarehe 20 hadi 23 Juni mwaka huu katika viwanja vya mnazi mmoja  jijini Dar es Salaam. Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa mikutano uliopo makao makuu ya ofisi hizo.
Naibu katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais Menejimenti  ya Utumishi wa Umma HAB Mkwizu (kushoto) akiongea na waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu maadhimisho ya siku ya utumishi wa Umma ya Umoja wa Mataifa na Afrika ambayo itafanyika kuanzia tarehe 20 hadi 23 Juni mwaka huu katika viwanja vya mnazi mmoja  jijini Dar es Salaam. Kulia ni Msemaji wa  Ofisi ya Rais Menejimenti  ya Utumishi wa Umma  Zamaradi Kawawa.
Baadhi ya Wakurugenzi wa Idara kutoka Ofisi ya Rais Menejimenti  ya Utumishi wa Umma wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu wa ofisi hizo HAB Mkwizu (hayupo pichani) wakati akiongea na waandishi wa Habari kuhusu maadhimisho ya siku ya utumishi wa Umma ya Umoja wa Mataifa na Afrika ambayo itafanyika kuanzia tarehe 20 hadi 23 Juni mwaka huu katika viwanja vya mnazi mmoja  jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya waandishi wa Habari wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais Menejimenti  ya Utumishi wa Umma HAB Mkwizu (hayupo pichani) wakati akiongea nao kuhusu maadhimisho ya siku ya utumishi wa Umma ya Umoja wa Mataifa na Afrika ambayo itafanyika kuanzia tarehe 20 hadi 23 Juni mwaka huu katika viwanja vya mnazi mmoja  jijini Dar es Salaam.
(Picha na Anna Nkinda – Maelezo).

0 comments:

Post a Comment