Rais Mwai Kibaki wa Kenya amewaita na kuwaagiza Waziri wa Nishati Kiraitu Murungi na Waziri wa Fedha Uhuru Kenyatta pamoja na maafisa wengine wa ngazi za juu kushughulikia haraka suala la uhaba wa mafuta ya petrol nchini humo linalohatarisha maendeleo ya uchumi.
Rais Kibaki ametoa agizo hilo kama kiongozi wan chi baada ya kuambiwa kuwa ukubwa wa tatizo hilo unachangiwa na madai kuwa wafanyabiashara wa mafuta wanaihujumu serikali ili iondoe udhibiti wa bei ya bidhaa hiyo.
Maafisa wa serikali wamefikia hatua ya kuwashutumu wafanyabiashara wa mafuta kwa kuhujumu uchumi na hata kuwatishia kuwa watawafutia leseni wafanyabiashara wasumbufu.
Maagizo hayo ya rais yamekuja huku kukiwa na ushahidi kuwa wafanyabiashara wa mafuta wameiingi sekta hiyo matatani wiki iliyopita kwa kufanya makusudi kutoweka akiba ya mafuta katika maghala yao.
Hatua ya rais Kibaki kuingilia tatizo hilo imefuatia uhaba wa mafuta ulioikumba nchi hiyo kuanzia Jumapili huku vituo kadhaa vya mafuta jijini Nairobi na maeneo ya nje vikikaukiwa mafuta hayo.

0 comments:
Post a Comment