SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Wednesday, May 18, 2011

CHAMELEON MATATANI KWA KUTISHA WAHUDUMU!!


Dr Jose Chameleon 
Siku chache  baada  ya  kupewa  idhini ya  kupiga  shoo  kwenye  ukumbi  maarufu wa  Monalisa Baa ulipo katikati ya jiji la Kampala King wa Muziki wa Kizazi Kipya pande hizo Dr Jose Chameleon ameingia matatani  baada  ya ‘kuwamwagia’ matusi ya nguoni wahudumu wanaoganga njaa katika bar hiyo.
Stori kutoka UG zinamwagika kuwa mwishoni mwa wiki iliyopita Chameleon alifika  kwenye  bar hiyo time Fulani ya  jioni akiwa  na washikaji zake kwa ajili ya ‘kuosha mbwa’ (kula bata) lakini aligeuka  mbogo na kuanza  kuwaporomoshea  maneno meusi wahudumu hao baada ya kupelekewa bili ya vinywaji na misosi aliyotumbua huku akionya  kusitisha  huduma ya  kupiga shoo hapo  endapo atazidi kusumbuliwa.
Kuona hivyo wahudumu hao  walinywea na  kuamua  kulipeleka  suala hilo  kwa  mmiliki wa  baa hiyo ambayo awali  ilikuwa ikijulikana kama  Mambo Jambo, kabla ya kubadilishwa jina na kuitwa Monalisa, kwa ajili ya  hatua zaidi.
Baada  ya taarifa  kumfikia  mmiliki wa baa hiyo ambaye ni mafanya biashara raia wa  Sudan  anayekwenda kwa jina  la (TITO) aliamua kumpigia  simu Chameleon na kutishia  kumshitaki huku akimwambia kuwa  kama  hata lipa bili hiyo atasitisha  ofa aliyompa ya kipiga shoo  katika ukumbi  huo kila Alhamis na  kumtupa  korokoroni.
“Siwezi kukuvumilia  kwa kitendo hicho, nitakushitaki na  nitasitisha makataba wetu wa kazi, najua kuwa nakufahamu wewe lakini siwatambui Loene Island Crew kwani  hawamo  kwenye makataba wetu  naomba ulipe bili hiyo mara moja na uache kuwatisha wahudumu wangu” alisema Tito kama alivyokaririw na The Daily Nation .
Na G5.

0 comments:

Post a Comment