Na Leon Bahati
Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye amejibu shutuma mbalimbali ambazo zimeelekezwa kwake na Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi huku akisema kauli za hivi karibuni za Umoja wa Vijana wa Chama hicho (UVCCM) ni matusi, kejeli na hatari kwa taifa.Sumaye (pichani) aliwaambia waandishi wa habari jana, Dar es Salaam kwamba CCM bado ni chama kinachotegemewa kuleta maendeleo kwa Watanzania siku zijazo lakini kauli za makada wake hao ni kali na zinaashiria kuwa hakina budi kusafishwa ili kirudi kwenye mstari.
"Future (mustakabali wa baadaye) ya CCM ni nzuri, ila kuna mambo lazima yafanyike. Udhaifu lazima tuuondoe," alisema Sumaye ambaye ni mwanachama mwanzilishi wa CCM na kuongeza:
"Chama kinapaswa kujivua magamba, nami nafikiri hii ndiyo njia sahihi ya kukijenga upya ili kiendane na misingi yake."
Hivi karibuni Baraza Kuu la UVCCM Taifa likitanguliwa na lile la Mkoa wa Pwani, walitoa kauli kali za kuwatisha viongozi wanaokikosoa chama hicho nje ya vikao, wakisema lengo lake ni kuharibu mustakabali wa CCM.
Umoja huo uliapa kuwa utafanya kampeni za kuhakikisha viongozi hao, uliodai kuwa wana malengo ya kupata Urais mwaka 2015, hawapati nafasi yoyote ya uongozi.
Sumaye ambaye alijiunga na Umoja wa Vijana wa Tanu wakati huo ukijulikana kama Tanu Youth League (TYL) mwaka 1969 alisema: "Kama UVCCM ingefanya kazi kwa vitisho na ubabe namna hiyo tangu awali, sidhani kama tungelikuwa na CCM tunayoiona leo."
Habari zaidi bofya: http://www.mwananchi.co.tz/

0 comments:
Post a Comment