Lile bifu la prodyuza anayemiliki Studio ya Sharobaro, Rahim Rummy Nanji ‘Bob Junior’ na stadi wa muziki wa Kizazi Kipya, Naseeb Abdul ‘Diamond’ limegeuka vita nzito likimjumuisha Miss Tanzania 2006/07, Wema Abraham Sepetu.
Akiwa katika mahojiano na Kituo cha kimoja cha redio mapema wiki hii, Bob Junior alimnanga Diamond ‘laivu’ hewani kuwa, amekwisha kimuziki na anajaribu kurudisha umaarufu kwa kutoka kimapenzi na Wema ambaye mbali na kuwa Miss Tanzania, pia ni moto wa kuotea mbali kunako Bongo movies.
Kabla ya Bob Junior kumwanika Diamond redioni, kuna maelezo kuwa, prodyuza huyo ‘alishatimba’ katika Kituo cha Polisi cha Oysterbay Kinondoni, Dar es Salaam na kumfungulia msanii huyo shitaka la kumtishia maisha.
Bob Junior alisikika akimchana Diamond: “Watu wanafahamu kuwa Diamond amekwisha kimuziki, anachojaribu kufanya ni kuutumia uhusiano wake na ‘kicheche’ Wema kurudisha umaarufu lakini hataweza kwa kuwa kila kitu kina mwisho wake.”
WEMA AJA JUU
Baada ya mahojiano ya Bob Junior yaliyojaa maneno mengi ya shombo kwa Diamond na Wema, mrembo huyo alitafutwa kwa ajili ya kujibu tuhuma kuwa yeye ndiye anampa ‘nyodo’ msanii huyo
ambapo alikuja juu mithili ya moto wa kifuu.
Wema alidai kuwa alikasirishwa ile mbaya na maneno ya Bob Junior huku akimshangaa kuhusisha bifu lao na uhusiano wake na Diamond.
Aliwaka: “Nimeshangazwa sana na hatua ya Bob Junior kunitaja kwenye bifu lake na mpenzi wangu. Ukweli ni kwamba nilikuwa simjui hata kidogo huyo Bob Junior leo imekuwaje akaniweka kwenye bifu nisilolijua?
“Kinachoniumiza zaidi ni yeye kunichafua na kuniita malaya, kama angekuwa amewahi kuwa mpenzi wangu, pengine angethibitisha ukicheche wangu. Nahisi kuna kitu kingine anachokitafuta na kama alikuwa ‘anamtaka’ Diamond ni bora aseme.”
Kauli hiyo ya Wema ilizua maswali mengi kwa mashabiki wa burudani Bongo waliotaka kujua Bob Junior ‘kumtaka’ Diamond kulimaanisha nini wakati wote ni ‘masharobaro’.
DIAMOND AJIPANGA KUJIBU MAPIGO
Kwa upande wake Diamond anayejiita Rais wa Wasafi aliliambia Amani kuwa, amesikia kila kilichosemwa na Bob Junior ‘Rais wa Masharobaro’ lakini anasubiri akutane na watu wake ili aamue cha kufanya kwa kuwa sasa anahisi kama ametangaziwa vita kamili.
“Nitazungumza baada ya kukutana na watu wangu wa karibu, kilichotangazwa sasa nahisi ni vita nzito ambayo damu itamwagika,” alisema Diamond.
SOO LATINGA OYSTERBAY
Awali gazeti hili lilipokea tetesi kuwa Bob Junior alikwenda polisi kuripoti tukio la kutishiwa maisha ambapo lilipomtafuta, alikuwa na haya ya kusema:
“Ni kweli nilikwenda kuripoti polisi baada ya kupata taarifa kutoka kwa mtu wangu wa karibu kuwa Diamond na ‘masela’ wake wamepanga kunifanyia kitu mbaya.
“Nilikwenda Kituo cha Polisi Oysterbay na kufungua jalada la kesi namba OB/RB/6303/2011-KUTISHIWA MAISHA. Hii ni kwa ajili ya kujihami ili siku nikipatwa na tatizo au nikifa, Watanzania wajue anayehusika ni nani.
“Kila nikikutana na Diamond na washikaji zake wamekuwa wakiniangalia kwa jicho baya hivyo kunikosesha amani.”
Jamaa aliendelea kusema kuwa, Diamond amekuwa akilazimisha bifu kwani kwa upande wake hana tatizo, pia siku zinavyozidi kwenda sifa ya Diamond inazidi kushuka kwa mashabiki ndiyo maana mwaka huu hakupata tuzo tofauti na mwaka jana alipotwaa Tuzo tatu za Kill na anatembea na wanawake maarufu ili aonekane yuko juu.
CHANZO CHA BIFU
Bifu la Bob Junior na Diamond lilianza miezi kadhaa iliyopita baada ya msanii huyo kumtaka prodyuza huyo kurekodi Kibao cha Gongo la Mboto ambapo alimjibu kuwa hawezi kufanya kazi hiyo kwani alikuwa anaumwa sikio.
Kitendo hicho kilimfanya Diamond kuanza kuzungumza kwenye vyombo vya habari kuwa mmiliki huyo wa Sharobaro alikataa kumrekodia kwa sababu alitaka alipwe fedha taslimu na hakuwa tayari kuifanya kazi hiyo.
KUTOKA AMANI
Ni vyema Bob Junior na Diamond wakakaa chini na kumaliza tofauti zao kwani huko ni kurudisha nyuma maendelea ya sanaa na wao kujishushia heshima mbele ya jamii.
CHANZO: BOFYA HAPA

0 comments:
Post a Comment