SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Thursday, April 14, 2011

SHARO MILIONEA AZOMEWA

SHARO MILIONEA
NA HEMED KISANDA
The Comedian Superstar Bongo, Hussein Mkiety, ‘Sharo Milionea’ ameonja joto ya jiwe baada ya kuzomewa na watoto wadogo alipokwenda katika maeneo yao ya kujidai. Muziki mzima unashushwa na Sharo Milionea mwenyewe, ambaye anaeleza kwamba wikiendi iliyopita alijongea kwenye kituo cha michezo ya watoto cha Funny City kilichopo Kigamboni, jijini Dar es Salaam alipokutana na kadhia hiyo. “Ebwana mtu mzima watoto noma, wamenitoa nishai wazi wazi. Unajua mimi nilienda pale kama kung’arisha macho tu, lakini madogo wakanitia aibu. “Nikiwa sina hili wala lile, mtoto mmoja aliniuliza aina ya suruali niliyokuwa nimeivaa, kwa kuwa sikuwa na uhakika kama ni ‘jinzi’ au ‘kadeti’, nilimjibu sijui, ndipo walipoanza kunizomea na kunizonga, sikuwa na namna mzee zaidi ya kukimbia,” alisema Sharo Milionea. Awali, Sharo alitinga katika viunga hivyo akiwa na wapambe wake, kwa lengo la kupumzika lakini watoto walipomuomba awachekeshe akakubali kutoa ‘free style’ lakini mwisho wake akaishia kuzomewa.
SOURCE: GLOBAL PUBLISHERS

0 comments:

Post a Comment