Dalili za nyota mwenye sauti ya dhahabu katika Muziki wa Kizazi Kipya, Peter Msechu kutinga ndani ya Shindano la Big Brother Africa zipo peupe, baada ya kuanza kwa mafanikio makubwa hatua za awali za kuelekea kwenye kinyang’anyiro hicho.
Msechu ambaye nyota yake ilianza kung’ara katika Shindano la Bongo Star Seach 2009 na kuibuka mshindi wa pili, kabla ya kutwaa nafasi kama hiyo kwenye kipute kingine cha Project Fame 2010 Nairobi, nchini Kenya, alisema haoni kikwazo kitakachomwangusha kutinga BBA.
“Najiamini sana na ni nina vigezo vyote, naamini lazima nitaingia BBA,” alisema Msechu kwa tambo.
Alisema tayari ameshachukua fomu na kilichofanyika ilikuwa ni mchujo wa kwanza, ambao uliwapitisha washiriki wanaochuana ili kupatikana mmoja atakayekwaa pipa kwenda kwa Madiba.
“Unajua katika zoezi la kufanya usaili kulikuwa na vyumba viwili na kila chumba kulikuwa na majaji kwa hiyo waliofanikiwa kupita vyumba vyote, ndiyo ambao wameingia katika hatua inayofuata, mimi ni mmoja wao.
“Tulikuwa washiriki wengi sana, lakini tuliofanikiwa kupita katika vyumba vyote siyo zaidi ya ishirini. Najiamini nina vigezo vyote, maana kwanza ni staa na pili naweza kuzungumza Kingereza vizuri,” alisema.
Mara kadhaa Tanzania imepeleka washiriki wake katika shindano hilo, lakini ni Richard Bezuidenhout pekee ndiye aliyeitoa nchi kimasomaso baada ya kutwaa taji hilo mwaka 2007. SOURCE: GLOBAL PUBLISHERS

0 comments:
Post a Comment