SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Monday, December 20, 2010

WILL SMITH KUTENGENEZA VIPINDI VYA TV 2011
Will Smith.
Pamoja na kuwa Will Smith anazo filamu kadhaa zilizopata umaarufu na kuvunja rekodi nchini Marekani zikiwemo mfululizo wa filamu za “Men in Black” na “I Am Legend” , lakini mwaka ujao staa huyo ambaye ni mmoja kati ya waigizaji wa Hollywood wenye asili ya afrika wenye kulipwa fedha nyingi anageukia katika kutengeneza vipindi vya luninga.
Imeripotiwa kuwa kinara huyo wa familia ya Smith ameungana na mtengeneza filamu wa China Eva Jin kubuni kipindi cha luninga kwa kampuni ya Fox kitakacho igiziwa katika mazingira ya China na kitahusu wanafunzi wa kike wa chuo wanaokabiliana na uhalifu.
Hata hivyo kama vile hiyo haitoshi, Will Smith pia yuko katika mchakato kutengeneza shoo ya luninga itakayohusiana na filamu yake iliyovuma ya mapenzi na vichekesho ya “Hitch”
Pamoja na kuwa mkakati huo wa pili wa filamu ya Hitch inaendana na uigizaji wa Smith wa vichekesho, wapenzi wa filamu na vipindi vya luninga wanahamu ya kuona jinsi hicho kipindi kitakachohusu uhalifu nchini China kitakavyokuwa chini ya Smith mwenyewe, kwani inaonekana kila kitu familia ya Smith itakachokigusa hujeuka kuwa dhahabu.

0 comments:

Post a Comment