SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Tuesday, December 14, 2010

PRODUCTION YATANGAZA FAINALI ZA KILI BSS 2010

Kampuni ya Benchmark Productions ambayo ni waandaaji wa shindano la kusaka na kuinua vipaji vya waimbaji lijulikanalo kama Bongo Star Search, wakishirikiana na mdhamini mkuu wa shindano hilo kampuni ya bia Tanzani (TBL) kupitia bia yake ya Kilimanjaro Premium Lager leo inatangaza rasmi tarehe ya kufanyika kwa fainali hizo.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, mkurugenzi wa Benchmark Production Bi. Rita Paulsen alisema fainali za shindano hili zinatarajiwa kufanyika Ijumaa hii tarehe 17 Dec 2010 katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City, kuanzia saa moja kamili usiku.
Ticket za shindano hili zimegawanyika katika makundi mawili ambapo kundi la kwanza ni kundi la viti maalum (VIP) ambazo zitauzwa kwa shilingi elfu Arobaini na tano (45,000/=) na kundi la pili ni kundi la viti vya kawaida ambazo zitauzwa kwa shilingi elfu ishirini (20,000/=).
Milango itafunguliwa kuanzia saa moja kamili jion na tiketi zinapatikana katika maduka yote ya shear Illusions, Biggy Respect, Ofisi za Benchmark Productions na katika ukumbi wwa mikutano wa Mlimani city ambapo fainali hizi zitafanyika.
Hundi ya milioni 30 ikionyeshwa na itamuendea mshindi atakayeshinda shindano hilo
Washiriki wa shindano hilo wakiwa wameshikilia hundi hiyo

0 comments:

Post a Comment