SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Monday, November 29, 2010

 Je, Ni Kwanini Mwamwindi Alimpiga Risasi Dr Kleruu? Nimefanya Mahojiano Na Mtoto Wa Mwamwindi ( 2)
Na Maggid Mjengwa, Iringa.
"Kleruu akamwuliza Mzee kwa ukali, ” Mbona mnafanya kazi leo siku ya Krismasi?”. Baba akamwomba Kleruu waende wakuzungumze nyumbani. Akamwambia mdogo wangu Mohammed aendelee kulima. Mzee akatangulia mbele, nyuma anamfuatia Kleruu. Kabla ya kufika kwenye nyumba yake wakayapita makaburi. Kleruu akamtamkia baba mzee Mwamwindi; ” Hapa ndipo unapozika mirija yako?” Alitamka hivyo huku akimtomasa tomasa mzee na kifimbo alichoshika mkononi.
Jambo hilo lilizidi kumkasirisha marehemu mzee. Akafika nyumbani kwake. Mlangoni alisimama mke wake mdogo. Inaonekana mzee alishafanya uamuzi. Jana yake alikwenda kuwinda. Hakupata mnyama. Bunduki yake moja aia ya riffle kati ya bunduki zake mbili ilikuwa bado ina risasi. Akamwambia mke wake mdogo huku Kleruu akiwa anasikia;
” Kanichukulie bunduki yangu”…… Endelea…
“ Je, aliposikia hayo Dr Kleruu alifanyaje?”
” Nadhani alipigwa na butwaa. Hakuamini kama baba angefikia hatua hiyo”
”Na ilikuwaje basi Mwamwindi alipoletewa bunduki?”
” Ilienda haraka, Mzee Mwamwindi akainua bunduki yake. Tayari ilikuwa loaded na risasa tangu jana yake alipotoka kuwinda. Kleruu aliinua mikono yote miwili kama mtu anayesalimu amri. Mwamwindi akampiga risasi ya kwapani. Kleruu akabaki hai. Akapiga risasi nyingine. Ikamwua pale pale.” Anasimulia Mzee Amani Mwamwindi.
Kinafuatia kimya. Anainama,..... Soma zaidi: http://mjengwa.blogspot.com

0 comments:

Post a Comment