Simba v Yanga SC
Na Saleh Ally, Mwanza
MASHABIKI wametakiwa kutoingia uwanjani wakiwa na kilevi cha aina yoyote ile wakati wa pambano la watani wa jadi Simba na Yanga, likalofanyika kesho jijini hapa.
Katika pambano litakalochezwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, mashabiki wameruhusiwa kunywa maji au juisi zilizo katika chupa za plastiki na si zaidi.
Akizungumza na Championi Ijumaa, Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha Soka Mwanza (MRFA), Nassib Mabrouk alisema wameamua kufanya hivyo kuongeza usalama zaidi na pia kupunguza bugudha.
“Hilo limeshapita, hatuwezi kumruhusu mtu kuingia na kilevi uwanjani kwa sababu za kiusalama. Kama mtu atakuwa anatumia kilevi, anaweza kushindwa kujitambua na kuanzisha vurugu. Hivyo ni marufuku.
“Tunatambua inaweza kuwa vigumu kudhibiti hilo moja kwa moja, kwa kuwa haujui mtu ametokea wapi kabla ya kuingia uwanjani. Lakini ndiyo hivyo, kwa uwanjani haitaruhusiwa,” alisema Mabrouk.
Pamoja na kudhibiti matumizi ya vilevi, uongozi wa MRFA umeonya watu wenye tabia ya kutoa lugha chafu hasa katika jukwaa la wageni wa heshima.
MRFA wamesema atakayefanya hivyo, atachukuliwa hatua kali za kisheria haraka na tayari wametangaza Mkuu wa Mkoa wa jiji la Mwanza, Abbas Kandoro kuwa mgeni rasmi.
Kumekuwa na mashabiki ambao hulazimisha kutumia lugha za matusi wakati wa mechi mbalimbali za Ligi Kuu ya Vodacom hali inayosababisha watu wengine kushindwa kwenda na familia zao uwanjani, hasa wake na watoto zao kwa kuhofia lugha hizo zinazotolewa bila ya ulazima wowote.

0 comments:
Post a Comment