Uchaguzi wa bunge la Afghanistan ulimalizika jana jioni ukigubikwa na machafuko na tuhuma za wizi wa kura.
Kamisheni Huru ya Uchaguzi ya Afghanistan imetangaza kuwa asilimia 40 ya watu waliotimiza masharti wameshiriki katika uchaguzi huo. Taarifa ya kamisheni hiyo imesema kuwa uchaguzi wa bunge umefanyika katika asilimia 92 ya ya vituo vya kupigia kura. Vilevile serikali ya Afghanistan imepongeza uchaguzi huo ikisema kwamba ulikua huru na wa haki. Hata hivyo mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan Staffan di Mistura ametangaza kuwa takwimu za idadi ya watu walioshiriki kwenye uchaguzi huo zinatia wasiwasi kutokana na hali mbaya ya usalama. Vilevile kumekuwepo kesi za wizi na udanganyifu katika vituo vingi na maeneo mbalimbali ya kupuigia kura.
Kundi la Taliban liliwataka wananchi kususia uchaguzi wa bunge wa Afghanistan na kutishia kushambulia vituo vya kupigia kura. Watu wasiopungua 10 wameuawa na wengine wengi kujeruhiwa katika ghasia zilizoandamana na uchaguzi huo.
0 comments:
Post a Comment