SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Friday, September 17, 2010

KIBAKA AKIONA CHA MOTO, ABANIKWA KAMA NDAFU!

  Na Hillary Shoo, Singida. KIBAKA mmoja ambaye hajafahamika jna lake wala makazi ameuawa kikatili na wananchi wenye hasira kali na kisha kuchomwa moto baada ya kufanya jaribio la kuvunja duka na kuiba bidhaa mbalimbali. Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia juzi majira ya saa 10 alfajiri katika eneo la Mwenge Manispaa ya singida ambapo kibaka huyo alikuwa na wenzake watano. Kwa mujibu wa watu walioshuuhudia tukio hilo walisema kuwa vibaka hao wakiwa watano waliika katika duka moja la Daniel Miyanji na kuanza kuvunja mageti ya duka hilo na kuanza kutoa idhaa mbalimbali zikiwmo bia nje. Akizunguma na gazeti hili mdogo wa mmiliki wa duka hilo Daniel Miyanji alisema akiwa amelala usiku huo alisikia kelelel za mbwa wa jirani wakibweka mfululizo. "Baada ya kuasikia kelele za mbwa wa jirani muda mrefu niliamka na kuchungulia dirishani na kuona watu wakitoa vitu dukani kwetu, ndipo nilimwamsha kaka yangu na atu wengine juu ya tukio hilo." alisema . Miyanji alisema kuwa hapo ndipo waliungana na kuanza kuwakurupua vibaka hao ambapo katika kurupushani hizo walifanikiwa kumkamata kibaka aliyekuwa ndani ya duka akitoa mali kwa wenzake na kuanza kushambuliana. Alisema kuwa kiaka huyo alikuwa akiwatisha kwa kisu lakini kutokana na umoja wa wananchi waliofika kutoa msaada baada ya kupiga makelele walimzidi nguvu na hatimae kuanza kumshambulia. "Mimi na kaka yangu tualiza kuwafukuzia wale vinbaka wengine ambao walikimbia na pesa ambazo hata hivyo idadi yake bado haijafahamika huku wananchi wakiendelea kumpa kibano kibaka huyo na hatimae kumchoma moto. Kamanda wa polisi Mkoani hapa Celina Kaluba amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwaba polisi wanafanya uchunguzi zaidi juu ya tukio hilo ikiwa ni pamoja na kuwasaka vibaka wengienwaliohusika katika tuko hilo. Hata hivyo wananchi wa maeneo ya jirani wamesema kuwa hiyo ni mara ya tatu kwa duka hilo kuvamiwa na vibaka na kisha mali kuchuliwa ambapo mwenye duka hiloa akiamka asubuhi anakuta duka jeupe na hivyo kumpunguzia nguvu kazi ya kujiletea maendeleo yake pamoja na familia yake. "Jamani sisi tumechoshwa na hawa wezi kila mara wanamwibia huyo kijana wa hili duka hebu angalieni mali yote imetolewa nje na kama sio kushiuka si angekuta hana kitu, tunasema tukikamata kibaka safai hii aaangalie mfano wa huyu mwenzao hatuna msaliamtume, polisi watakuja kuchukua majivu tu."Alissisistiza mama mmoja jirani na eneo hilo la tukio.

0 comments:

Post a Comment