Makundi 11 ya Kipalestina yamekutana nchini Syria na kuchukua msimamo mmoja wa kupinga kufanyika mazungumzo ya moja kwa moja au yasiyokuwa ya moja kwa moja na utawala wa Kizayuni wa Israel. Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas pamoja na makundi mengine 10 yamesisitiza kupinga kufanyika mazungumzo ya aina yoyote ya kufatuta amani na utawala ghasibu wa Israel. Taarifa hiyo imetolewa huku Rais Mahmoud Abbas wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina akitarajiwa kukutana na David Hill Mjumbe wa Marekani katika masuala ya Mashariki ya Kati huko Ramallah, kwa shabaha ya kumrubuni Mahmoud Abbas arejee tena kwenye mazungumzo eti ya amani na Wazayuni. Makundi hayo yameeleza kuwa, kukubali kufanya mazungumzo na Wazayuni, kuna maana ya kukubali masharti ya Washington na Tel Aviv ya kutokomeza kabisa haki za Wapalestina.
Monday, August 16, 2010
Wapalestina wanapinga kufanyika mazungumzo ya aina yoyote na Wazayuni
Posted by
Ally Shaaban Mgido's
at
Monday, August 16, 2010
Email This
BlogThis!
Share to Twitter
Share to Facebook
0 comments:
Post a Comment